Search
Close this search box.
Africa

Tulipokuwa watoto tuliulizwa na wazazi wetu ni kazi zipi tungependa kufanya mara tu tunapokuwa watu wazima. Mara nyingi tulitaja kazi za kuvutia kama vile daktari, wakili, rubani, mwalimu n ahata muuguzi.

Lakini tunapokuwa watu wazima tunaona wazi kuwa haikuwa rahisi kufikia ndoto zetu iwe ni kutokana na kukosa hela ya shule au hata nafasi ya kutimiza ndoto hizo.

Mfumuko wa bei na hivi maajuzi mlipuko wa janga la Corona umewafanya watu wengi kupoteza ajira zao.

Lakini unafahamu kuwa zipo kazi ambazo unaweza kufanya bila kuhitaji stakabadhi za chuo kikuu au kuhitaji tajriba ya miaka mingi.

Mfano kuna kazi ya kusukuma watu kuabiri treni, kazi hii inapatikana mjini Tokyo nchini Japan. Japan ni taifa la watu wenye bidii, ili kuhakikisha kuwa watu wanafika kazini kwa wakati unaofaa Japan imeajiri watu maalum wanaofahamika kama Oshiya , jukumu lao ni kuwakusukuma abiria kuingia kwenye treni ili watu wasichelewe kazini na treni zote ziende kwa wakati unaostahili.

Maafisa maalum ‘Oshiya’ wakusukuma watu kuabiri treni

Kazi nyingine ambayo unaweza kufanya bila kuhitaji tajriba wala stakabadhi ni ya kusimama kwenye foleni, iwe ni katika benki, dukani au hata katika kumbi za sinema. Unalohitajika kufanya ni kusimama kwenye foleni iwapo mteja hana wakati huo au ana shughuli nyingine za kufanya.

Kazi ya tatu unayoweza kufanya ni kuwa mtaalamu wa kulala. Katika kazi hii unapata ajira katika viwanda vya kuzalisha magodoro. Kazi yako itakuwa kutathmini ubora wa magodoro.

Kazi nyingine ni ya kutathmini ubora wa manukato ya kukabiliana na harufu ya jasho yaani ‘deodorant’. Katika kazi hii unahitajika kunusa makwapa ya watu waliopaka mafuta hayo ili kukadiria uwezo wa deodorant kukabiliana na harufu ya jasho.

Kazi ya kunusa makwapa baada ya kupaka deodorant

Zipo kazi nyingi tu ambazo hazihitaji stakabadhi, zingine zinahitaji tu uwe unapenda kula. Ipo kazi ya kuonja chakula cha wanyama kama vile mbwa na paka.

Hii nyingine ni kazi ambayo imekuwepo katika nchi nyingi Afrika, ikiwemo Nigeria na Kenya. Kazi ya mtaalamu wa kuomboleza. Watu hawa huajiriwa wakati wa matanga ili kuwasaida waliofiliwa kuomboleza.

Waombolezaji wa kulipwa.

Comments are closed