Umoja wa Mataifa Watangaza Njaa Kuwa Janga Kuu huko Gaza Kwa mara Ya Kwanza Mashariki ya Kati

Umoja wa Mataifa kupitia mfumo wa IPC umetangaza rasmi kuwepo kwa njaa kali katika Ukanda wa Gaza, ikiwa ni mara ya kwanza kutokea Mashariki ya Kati.

Umoja wa Mataifa Yatangaza Njaa Kuwa Janga Kuu huko Gaza Kwa mara Ya Kwanza Mashariki ya Kati

Takriban watu nusu milioni wanakabiliwa na hali ya “njaa, ufukara na kifo,” huku zaidi ya milioni moja wakiwa katika hatari ya dharura ya chakula.

Ripoti ya IPC inaonyesha kuwa vigezo vyote vitatu vya kutangaza njaa, ukosefu wa chakula cha kutosha, utapiamlo mkali, na vifo vinavyohusiana na njaa, vimefikiwa Gaza City.

Maeneo ya Deir Al-Balah na Khan Younis yanatarajiwa kuingia katika hali hiyo kufikia Septemba ikiwa misaada haitafika kwa haraka.

Mkuu wa misaada wa UN, Tom Fletcher, amesema njaa hii “imesababishwa na ukatili, ikahalalishwa kwa kisasi, na kudumishwa kwa kutojali.” Aliongeza kuwa chakula kipo karibu, lakini kinaendelea kuzuiliwa mipakani na vizuizi vya Israel.

Wakati Israel ikikanusha kuwepo kwa njaa, mashirika ya kibinadamu yanatoa wito wa kusitisha mapigano mara moja, kuachilia mateka wote, na kuruhusu misaada kufika bila vizuizi.

Katibu Mkuu wa UN António Guterres ameita hali hii “janga la kibinadamu linalosababishwa na binadamu,” akisisitiza haja ya hatua za haraka za kimataifa.