Nchi za BRICS, kifupi cha wanachama tano Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini zinakutana kwa siku tatu kwa mkutano wa kilele huko Johannesburg kuanzia Jumanne.
Haya ndiyo unayohitaji kujua kuhusu BRICS:
Hapo awali BRIC, kifupi cha Brazil, Urusi, India, na Uchina, ilikutana kwa mara ya kwanza mnamo Juni 2006 na ilirasimishwa mwaka huo huo mnamo Septemba.
BRIC ilifanya mkutano wake wa kwanza wa kilele mwaka 2009 huko St Petersburg, Russia, na kukubali Afrika Kusini kama mwanachama wake mwaka 2010 na kubadili jina la kundi hilo na kuwa BRICS (Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini).
Wakiwakilisha asilimia 23 ya pato la taifa la dunia (GDP) na asilimia 42 ya idadi ya watu duniani, muungano huo uliundwa ili kuongeza utulivu wa kiuchumi na kisiasa miongoni mwa nchi wanachama wake. Pia inaangazia kuongezeka kwa maendeleo na biashara ya kimataifa kote duniani.
Wanachama wa kambi hiyo hukutana kila mwaka na uenyekiti wa mzunguko wa mwaka mmoja kutoka kila taifa.
Huku mkutano wake wa kilele wa 15 ukifanyika mjini Johannesburg kuanzia Agosti 22 hadi 24, 2023, kikundi hicho kinataka kujumuisha wanachama wengine wa nchi.
Huu utakuwa ni mkutano wa kwanza wa kilele wa BRICS tangu janga la COVID-19 kukumba duniani
Kama mwenyekiti wa 2023 wa BRICS, Afrika Kusini inasema zaidi ya nchi 40 zimeonyesha nia ya kujiunga na umoja huo, ili kufungua faida kama vile kuongezeka kwa biashara na uwekezaji.
Nchi zikiwemo Iran, Saudi Arabia, Falme za Kiarabu, Argentina, Algeria, Bolivia, Indonesia, Misri, Ethiopia, Cuba, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Comoro, Gabon na Kazakhstan,
Nyingine ni; Vietnam, Bahrain, Palestina, Thailand, Nigeria, Senegal, Malawi, Venezuela, na Belarusi miongoni mwa zingine.