Upinzani Tanzania walia wagombea wao wameenguliwa kushiriki uchaguzi

Zikiwa zimebaki siku 16 watanzania kuchagua viongozi wao kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, chama cha ACT Wazalendo na Cgadema vinaendelea kulia kutokana na wagombea wao kuenguliwa.

Katika taarifa kwa vyombo vya Habari mapema leo, cha ACT-Wazalendo kimesema wagombea wake 51,423 wameenguliwa.

Kwa upande, chadema kupitia mkurugenzi wake wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje John Mrema amesema wagombea waliokuwa wameteuliwa awali wanaendelea kuenguliwa hadi sasa. Mrema ametoa mfano wa Manispaa ya Iringa, ambapo amesema walioteuliwa wote, wameenguliwa.
Mrema pia amesema Maeneo maengine ambayo wagombea wa Chadema wameenguliwa Tarime Vijijini, Sumbawanga, musoma, sengerema, Kagera, Igunga, Rufiji, Tunduma, Morogoro na Shinyanga.

Chadema inasema kibaya Zaidi ni kuwa wagombea hao hawapewi pingamizi kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi.
ACT Wazalendo na Chadema tayari kimemjulisha Waziri wa Tamisemi Mohamed Mchengerwa kuhusu tukio hilo ambalo wanasema limewastaajabisha. Wameta wote walioenguliwa kurejshea mara moja.
Uchaguzi wa serikali za mitaa zitafanyika tarehe 27 mwezi huu.