WanaJeshi wanaotawala Mali umeamuru kusimamishwa mikutano zote za kisiasa kote nchini, ukisema kuwa hatua hiyo inahitajika ili kudumisha utulivu na amani ya raia.
Katika taarifa ya kiongozi wa kijeshi Kanali Assimi Goita, iliyosomwa na msemaji wa serikali Kanali Abdoulaye Maiga, Kanali Goita amesema kuwa “kwa ajili ya utulivu wa umma, shughuli za vyama vya siasa na shughuli za kisiasa zimesimamishwa kote nchini, hadi pale itakapoamuriwa tena”.Mali yaitaka MINUSMA kuondoka nchini humo mara moja
Amri hiyo inatolewa baada ya zaidi ya vyama 80 vya kisiasa na mashirika ya kiraia mnamo Aprili mosi, kutoa taarifa ya pamoja ya kutaka uchaguzi wa rais kufanyika “haraka iwezekanavyo” na kukomesha utawala wa kijeshi.
“Tutatumia njia zote za kisheria na halali kurejesha utaratibu wa kawaida wa kikatiba katika nchi yetu,” ilisema taarifa ya pamoja iliyotiwa saini zaidi na watu zaidi ya 20, ukiwemo muungano mkubwa wa upinzani na chama cha rais wa zamani aliyepinduliwa.
Nchi hiyo ya Afrika Magharibi imetawaliwa na wanajeshi tangu mapinduzi ya mwaka 2020 na 2021, huku hali mbaya ya usalama ikichangiwa na mzozo wa kibinadamu na kisiasa.