Vijana nchini kenya almaarufu Gen Z wamepanga kufanya maandamano kubwa Zaidi jijini Nairobi siku ya alhamisi tarehe 18. Kulingana na taarifa mapango yanayosambazwa katika mitandao ya kijamii, Vijana wamehamasishana kukutana katika bustani la uhuru jijini Nairobi.
Kulingana na bango hilo lenye kauli mbiu ‘’Vamia uhuru park, vijana wanaomba kubeba vifaa vya kujikinga, chakula, maji, kuvalia nguo za kuleta joto, blanketi na vifaa vya huduma ya kwanza.
Maandamano hayo ya kesho kama ilivyonakili kwenye bango hilo ni kulaani ukatili wa polisi ambapo baadhi ya waandamanji wameuawa.
Vijana Zaidi ya milioni tano kutoka maeneo taofauti hususan jijini Nairobi na viunga vyake wameombwa kufika uhuru park. Baada ya mkutano mfupi, kundi hilo limeapa kufanya maandamano ya lazima hadi ikulu ya Nairobi wakisisitiza lazima Rais William Ruto aondoke madarakani.
YES. Occupy Uhuru Park and Everywhere until Zakayo falls. Make it huge. Let it be a marathon peaceful protests without a break. Do it throughout the country. Let’s wear them out. #RutoMustGoNow #RutoMustGo pic.twitter.com/duV7kOkbAA
— Dr. Miguna Miguna (@MigunaMiguna) July 17, 2024