Visa 5,375 vya mimba za utotoni vyaripotiwa katika wilaya ya Kwania,Uganda mwaka wa 2021.

Wilaya ya Kwania nchini Uganda imeripoti visa vingi vya mimba za utotoni katika kipindi cha miezi 21, hali hiyo ikihatarisha masomo ya wasichana hao.

Taarifa hiyo ilichapishwa kwenye data iliyowasilishwa kwa msaidizi wa utafiti, Moses Opio wakati wa kikao cha robo mwaka cha kamati ya uongozi wa wilaya uliofanyika Jumanne na Plan International Uganda.

Kulingana na data, takriban visa 5,375 vya mimba za utotoni viliripotiwa katika wilaya ya Kwania kati ya Januari 2020 hadi Septemba 2021.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa, visa 3,046 vilirekodiwa mwaka wa 2021 na visa 2,329 vilirekodiwa mwaka wa 2020.

Moses Opio, afisa wa maslahi analaumu wazazi na mfumo wa haki usiofaa kwa hali ilivyo kwa sasa, akiongeza kuwa iwapo wazazi wangetimiza majukumu yao, wasichana hao hawangepata mimba hizo za utotoni.

Mwenyekiti wa wilaya ya Kwania Geoffrey Alex Ogwal, amasema kuongezeka kwa mimba za utototni kunatokana na wazazi kutojukumika, kutaka mahari, umasikini na tamaduni duni.Ameitaka serikali kushughulikia maslahi ya polisi ili waweze kukabiliana na uovu huo.

Emmanuel Oscar Ogwang,Mkurugenzi wa Safe Aids Uganda, shirika lisilo la kiserikali, linasema linapitia changamoto nyingi na polisi wanaoshughulika na kesi za unyanyasaji wa kingono dhidi ya watoto.

Bwana Ogwang, anasema kuwa juhudi zao za kutaka washukiwa wa unyanyasaji wa kingono kuchukuliwa hatua hazijafaulu kwasababu, maafisa wa polisi hutaka kupewa hongo na washukiwa ili kesi ikose kuendelea.

Leonard Agum, Afisa wa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya ya Kwania, anawatakla wazazi kujenga uhusiano wa karibu na watoto wao ili kupunguza ongezeko la visa vya miba za utotoni katika wilaya hiyo.