Search
Close this search box.
Europe
Jengo lililoshambuliwa na roketi za Urusi katika mji wa pili kwa ukubwa Kharkiv mnamo Machi 3, 2022. (Photo by Sergey BOBOK / AFP)

Baada ya Urusi kuizingira Ukraine kwa makumi ya maelfu ya wanajeshi, Urusi ilivamia jirani yake mapema Februari 24, na kuanzisha mzozo mbaya zaidi barani Ulaya katika miongo kadhaa.

Urusi yavamia

Alfajiri ya Alhamisi iliyopita, Rais wa Urusi Vladimir Putin alitangaza “operesheni maalum ya kijeshi” ‘kuwaondo washirika wa Nazi’ na kuunga mkono jimbo linalotaka kujitenga na linaloungwa mkono na Urusi.

Akatishia nchi zinazoingilia mzozo huo ‘kufanyiwa mambo mabaya ambayo hawajawahi kushuhudia mbeleni”.

Uvamizi wa kiwango cha juu ukaanza mara moja na mashambulio ya anga na mizinga kwenye miji kadhaa.

Vikosi vya Urusi pia vikadhibiti kwa muda uwanja wa ndege ulioko viungani mwa mji wa Kyiv.

Ukraine yatangaza sheria ya kijeshi na kukata uhusiano na Urusi.

Wakimbizi watorokea mataifa mengine

Wakimbizi wamiminika kutoka Ukraine kuenda nchi za Poland, Hungary, Romania, Moldova na Slovakia.

Ndani ya wiki moja zaidi ya wakimbizi milioni moja wakimbilia nchi jirani.

Mnamo Februari 25, nchi za Ulaya zanaanza kufunga anga zao kwa mashirika ya ndege ya Urusi na wanachama wa EU waanza kuwawekea vikwazo Putin na Waziri wa Mambo ya Nje Sergei Lavrov.

Ukraine yawazuia wanajeshi wa Urusi

Vikosi vya Ukraine viliweka upinzani mkali kuliko ilivyotarajiwa, na kukatisha mipango ya Urusi ya kunyakua miji yao kwa haraka.

Katika mfululizo wa video za selfie Rais Volodymyr Zelensky aapa kukaa nchini na kuongoza vita dhidi ya Urusi.

“Ninahitaji risasi, sio gari kuondoka nchini mwangu,” aliwaambia Wamarekani, wanaojitolea kumhamisha.

Huku hofu kwamba Kyiv itaanguka mikononi mwa wanajeshi wa Urusi ikishindwa kutimia, video zinaibuka zikionyesha Waukraine wakijaribu kuzuia magari ya wanajeshi wa Urusi kwa mikono yao, au kuwakemea askari wa Urusi waliojaa mitaani.

Siku ya Jumamosi, Urusi iliamuru wanajeshi wake kusonga mbele ‘kutoka pande zote,’

 Tishio la shambulizi la nyuklia

Siku ya Jumapili, Putin aliongeza mvutano zaidi kwa kuweka vikosi vya nyuklia vya Urusi katika hali ya tahadhari.

Mamia ya maelfu ya watu kote ulimwenguni washiriki katika maandamano ya kuunga mkono Ukraine.

Waamerika waandamana kupinga uvamizi wa Ukraine Joe Raedle/Getty Images/AFP (Photo by JOE RAEDLE / GETTY IMAGES NORTH AMERICA / Getty Images via AFP)

EU inasema itatumia karibu euro nusu bilioni kuipatia Ukraine silaha huku mataifa wanachama yakiahidi msaada wao wa kijeshi.

Vikwazo vyawekwa kuondoa baadhi ya benki za Urusi kutoka kwa mfumo wa malipo wa benki wa SWIFT.

Uvamizi huo pia umeibua fikra mpya katika sera ya ulinzi ya Ujerumani, huku Berlin ikiongeza matumizi yake ya kijeshi.

Kharkiv yashambuliwa mazungumzo yakiendelea

Duru ya kwanza ya mazungumzo kati ya Kyiv na Moscow yaliyofanyika kwenye mpaka wa Ukraine na Belarus siku ya Jumatatu hayakufanikiwa.

Wakati mazungumzo hayo yakiendelea, wilaya za mji wa pili wa Ukraine wa Kharkiv zipigwa makombora  na roketi.

Zelensky anatoa wito kwa nchi yake kupewa uanachama wa ‘haraka kujiunga na’ EU.

Mjini Kyiv, jeshi linasema kuwa limepambana na majaribio kadhaa ya vikosi vya Urusi kuvamia viunga vyake.

Sarafu ya Urusi Ruble yapoteza thamani huku benki kuu ya Urusi ikiongeza kiwango cha riba yake maradufu ili kujaribu kuisaidia sarafu hiyo.

Mafanikio ya Urusi maeneo ya kusini

Siku ya Jumanne, picha za satelaiti zinaonyesha msafara mkubwa wa magari ya Urusi yakielekea Kyiv.

Urusi yatimuliwa kutoka kwa Kombe la Dunia la 2022 huku vikosi vyake vikizunguka mji wa kusini wa Kherson pamoja na bandari ya Bahari ya Black Sea ya Mariupol.

Shambulio la kombora laharibu ukumbi wa jiji la Kharkiv.

Wakati wa hotuba yake Rais Joe Biden anamtaja Putin kama ‘dikteta’

Vyombo vya habari vya Urusi vyanyamazishwa

Siku ya Jumatano, majeshi wa kutumia parachuti wa Kirusi watua Kharkiv, eneo ambalo linaendelea kushambuliwa kwa makombora,  majengo ya chuo kikuu ni miongoni mwa majengo yaliyoshambuliwa.

Urusi yaifungia chaneli huru ya runinga na kituo cha redio kupeperusha matangazo kuhusu vita hivyo siku ya Jumatano.

Kwa mara ya kwanza, Moscow yatoa idadi ya vifo ya wanajeshi wake, ikisema 498 wameuawa.

Mazungumzo mapya –

Wiki moja baada ya mashambulizi kuanza, Warusi wateka Kherson, jiji kuu la kwanza kuanguka.

Maafisa wa Ukraine na Urusi wanasafiri hadi mpaka wa Belarus na Poland kwa duru ya pili ya mazungumzo, ambapo wanakubali kuunda njia maalum kusaidia watu kutoroka vita hivyo.

Putin anasema kwamba jeshi la Urusi limefaulu kuingia ndani zaidi katika miji ya Ukraine na kuwa kila kitu kinakwenda “kulingana na mpango” huku akifanya mkutano na baraza lake la usalama.

Comments are closed