Waasi wa M23 wauteka mji wa Goma

Waasi wa kundi la M23 wameingia kwenye kitovu cha mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Goma, masaa kadhaa baada ya kutangaza kutwaa udhibiti wa mji huo muhimu.

A woman carries a mattress and other belongings on her head as she flees from Kibati, where fighting has intensified, towards the city of Goma on January 26, 2025. The M23 armed group has seized further territory in the east of the Democratic Republic of Congo and on Sunday was continuing to tighten its grip on provincial capital Goma, which is almost surrounded by fighting. (Photo by Jospin Mwisha / AFP)

Hadi sasa haijawa wazi endapo waasi hao wanaoungwa mkono na Rwanda wamefanikiwa kuutwaa mji huo wote ulio kwenye ufukwe wa Ziwa Kivu, lakini vyanzo mbalimbali vililiambia shirika la habari la Reuters kwamba angalau kwenye uwanja wa ndege, bado wanajeshi wa Umoja wa Mataifa na wa serikali wanaonekana.

Tryphon Kin-Kiey Mulumba, mwenyekiti wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga, alisema bado jeshi la Kongo lilikuwa ndilo linaloudhibiti uwanja huo wa ndege.

A woman carries a mattress and other belongings on her head as she flees from Kibati, where fighting has intensified, towards the city of Goma on January 26, 2025. The M23 armed group has seized further territory in the east of the Democratic Republic of Congo and on Sunday was continuing to tighten its grip on provincial capital Goma, which is almost surrounded by fighting. (Photo by Jospin Mwisha / AFP)

“Kuna mkanganyiko kwenye mji huu, hapa karibu na uwanja wa ndege tunawaona wanajeshi. Sijawaona wapiganaji wa M23 bado. Pia kuna matukio ya uporaji kwenye maduka.” Mmoja wa wakaazi waliokuwa wakikimbia uvamizi huo wa M23 aliliambia shirika la habari la Reuters.

Kufikia mchana wa leo, milio ya risasi ilikuwa inasikika karibu na uwanja huo wa ndege, kwenye kitovu cha mji na karibu na mpaka wa Rwanda.

Picha za video ambazo shirika la habari la AFP lilishindwa kuzithibitisha zinaonesha wakaazi wakishiriki kwenye uporaji wa maduka nje ya maghala ya uwanja wa ndege na watu wenye silaha nzito wanaoaminika kuwa waasi wa M23 wakirandaranda kwenye viunga cha kaskazini vya Goma.

Residents carry their belongings as they flee from Kibati, where fighting has intensified, towards the city of Goma on January 26, 2025. The M23 armed group has seized further territory in the east of the Democratic Republic of Congo and on Sunday was continuing to tighten its grip on provincial capital Goma, which is almost surrounded by fighting. (Photo by Jospin Mwisha / AFP)

Haikuwa rahisi kuthibitisha kwa haraka nani anayehusika na ufyatuaji risasi, lakini mkaazi mmoja aliliambia shirika la habari la Reuters kwamba huenda hizo zilikuwa risasi za onyo na sio mapigano.

 

Awali waasi hao walikuwa wamewaamuru wanajeshi wa serikali kujisalimisha ifikapo saa tisa usiku wa leo Jumatatu na tayari wanajeshi 100 wa Kongo walishasalimisha silaha zao kwa wanajeshi wa Uruguay wanaohudumu kwenye Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa nchini humo, MONUSCO, kwa mujibu wa jeshi la Uruguay.

Wafanyakazi wa MONUSCO na familia zao wanaendelea kuhamishwa kuelekea mpaka wa Rwanda, ambako mabasi kumi yalikuwa yakiwangoja kuwasafirisha.

A family pushes a Chukudu loaded with mattresses and other belongings as they flee from Kibati, where fighting has intensified, towards the city of Goma on January 26, 2025. The M23 armed group has seized further territory in the east of the Democratic Republic of Congo and on Sunday was continuing to tighten its grip on provincial capital Goma, which is almost surrounded by fighting. (Photo by Jospin Mwisha / AFP)

Hayo yakijiri, Rais William Ruto wa Kenya, ambaye kwa sasa ndiye mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ameitisha mkutano wa viongozi wakuu wa jumuiya hiyo kujadili hali ya Kongo, kwa mujibu wa katibu mkuu wa wizara ya mambo ya nje ya Kenya, Korir Sing’Oei.

Jana Jumapili, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliitisha kikao cha dharura kuizungumzia hali hiyo na baadaye Marekani, Ufaransa na Uingereza kulaani kile walichosema ni uungaji mkono wa Rwanda uliowawezesha waasi wa M23 kusonga mbele.

Kigali imekanusha kauli hiyo iliyosema haijatowa suluhisho lolote na badala yake imeilaumu Kinshasa kwa kuchochea hali ya sasa.