Waasi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamewauwa watu 16 na kuwajeruhi wengine saba na kuchoma magari wakati wa uvamizi wa usiku katika eneo lenye hali tete la Mashariki, Shirika la Msalaba Mwekundu na wenyeji walisema Jumatatu.
Shambulio hilo lilitokea Jumapili jioni huko Bulongo katika jimbo la Kivu Kaskazini, kulingana na rais wa vijana wa kijiji Andika Miheko, ambaye alilaumu kundi mashuhuri la Allied Democratic Forces (ADF).
“Walichoma magari matano na watu waliokuwa ndani waliteketezwa kwa moto,” alisema na kuongeza kuwa vurugu hizo ziliendelea hadi asubuhi ya Jumatatu.
Sahani Kambale, mkuu wa tawi la Msalaba Mwekundu la Bulongo, alisema kundi la kibinadamu liligundua miili 16 baada ya shambulio hilo.
Watu saba pia walijeruhiwa.
Mmoja wa waliouawa ni mfanyakazi wa Msalaba Mwekundu, ambaye alipigwa risasi alipokuwa akijaribu kutoroka, kwa mujibu wa katibu wa eneo wa shirika hilo, Albert Ndungo.
Shambulio la hivi punde ni la nne kwa Bulongo kulaumiwa na ADF tangu 2020.
Ikielezewa na kundi la Islamic State kama mshirika wake wa ndani, ADF imeshutumiwa kuua maelfu ya raia mashariki mwa DRC yenye machafuko.
Waasi wa ADF pia waliwauwa raia 27 katika shambulio huko Kivu Kaskazini Jumamosi, kulingana na jeshi na wengine.
Tangu Mei mwaka jana, vikosi vya usalama vya Congo vimeendesha utawala katika Kivu Kaskazini na nchi jirani ya Ituri katika jitihada za kuangamiza maelfu ya makundi ya waasi wanaofanya kazi huko.
Mauaji ya raia yanaendela.