Watu wanaoshukiwa kuwa wanajihadi waliwauwa takriban raia 50 wa Burkina Faso, gavana wa eneo la Mashariki alisema Alhamisi, katika shambulio la hivi punde katika taifa hilo.
Raia hao kutoka Madjoari walifariki siku ya Jumatano wakijaribu kukimbia kizuizi cha wanajihadi, alisema Kanali Hubert Yameogo kwenye taarifa, akiongeza kuwa idadi hiyo ilikuwa ya muda.
Walionusurika waliambia AFP kwa njia ya simu kuwa walikuwa wakijaribu kuwatoroka washambuliaji.
“Watu walizuiliwa na kuuawa na magaidi,” mmoja wa walionusurika alisema.
“Wafu wote walikuwa wanaume.” Gavana wa eneo hilo alisema: “Operesheni za usalama zinaendelea ili kurejesha amani.”
Moja ya nchi maskini zaidi duniani, Burkina Faso imetikiswa na uvamizi wa wanajihadi tangu 2015, huku vuguvugu hilo likihusishwa na Al-Qaeda na kundi la Islamic State.
Zaidi ya watu 2,000 wameuawa na milioni 1.8 wamekimbia makazi yao.
Jumapili iliyopita watu wanaoshukiwa kuwa wanajihadi waliwaua watu 11 katika vijiji viwili kaskazini mwa Burkina.
Na Alhamisi iliyopita, wanajeshi 11 na watu 15 wenye silaha walikufa katika shambulio lingine, mashariki mwa nchi, jeshi lilisema.
Mnamo mwezi Januari wanajeshi walioasi, waliokasirishwa na hasara iliyotokana na mashambulizi ya wanajihadi, walimpindua rais Roch Marc Christian Kabore.
Luteni Kanali Paul-Henri Sandaogo Damiba alichukua madaraka na kufanya mzozo wa usalama kuwa kipaumbele chake.
Lakini baada ya ghasia kutulia, kuongezeka kwa mashambulizi kumesababisha vifo vya zaidi ya watu 200 miongoni ikiwa ni raia na wengine kutoka vikosi vya usalama.