Naibu Rais William Ruto wa Kenya Kwanza na Raila Odinga wa Muungano wa Azimio La Umoja walitoa wito wao wa mwisho kwa Wakenya, siku ya Jumamosi, huku wapiga kura wakijiandaa kwa uchaguzi.
Naibu Rais William Ruto aliongoza muungano wake wa Kenya Kwanza katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo huku mpinzani wake Raila Odinga wa Azimio la Umoja One-Kenya akiwa katika uwanja wa Kasarani.
Wawili hao wamezindua manifesto zao kwa Wakenya wakiwa na ahadi za afya, Elimu miongoni mwa mambo mengine mazuri iwapo watachaguliwa.
Mgombea Urais wa Chama cha Roots George Wajackoya pia alihitimisha kampeni zake jijini Nairobi kwa wito kwa wakenya kumpigia kura siku ya Jumanne. Wajackoya alipuuzilia mbali madai kuwa anajiunga na muungano wa Azimio. Mgombea mwenza wake Justina Wamae alithibitisha kwamba maono yao ya kubadilisha hali ya nchi iko mbioni.
Katika maeneo mengine ya Nairobi, mgombea Urais wa Agano David Mwaure aliwataka Wakenya kuunga mkono azma yake. Alisema ni yeye pekee anayeweza kuaminiwa kupambana na ufisadi katika nchi hii