Search
Close this search box.
Africa

Nigeria itakwenda uchaguzini Februari 2023 kumchagua mrithi wa Rais Muhammadu Buhari ambaye ataondoka uongozini baada ya kuhudumu kwa mihula miwili.

Kabla ya kura hiyo muhimu, vyama 18 vinatarajiwa kufanya mchujo ili kuwachagua watakaopeperusha bendera ya urais ifikapo Juni 3 kulingana na miongozo ya mamlaka ya uchaguzi INEC.

Vyama viwili vinavyoongoza — chama tawala cha All Progressives Congress (APC) na chama kikuu cha upinzani Peoples Democratic Party (PDP)– vitafanya mchujo wao kuanzia wikendi hii.

Chini ya mpango usio rasmi wa kusawazisha vyeo kulingana na kabila na kanda za Nigeria, mamlaka ya kuongoza nchi huzungushwa kati ya Nigeria kaskazini yenye Waislamu wengi na kusini yenye Wakristo wengi.

Wagombea 25 kutoka chama cha APC wanagombea tikiti, lakini washindani wakuu ni:

Yemi Osinbajo

Makamu wa Rais, Yemi Osinbajo ni profesa wa chuo kikuu na wakili mkuu amekuwa naibu wa Buhari tangu 2015. Mkristo huyo mwenye umri wa miaka 65 kutoka kusini magharibi mwa Nigeria ameahidi kuendelea na sera za bosi wake iwapo atashinda kuwa rais.

Anachukuliwa kuwa mshirika wa zamani wa gavana wa zamani wa Lagos Bola Ahmed Tinubu, mgombea mwingine kutoka eneo hilo, ingawa wanaume hao wawili sasa wanashindana katika mchujo.

Bola Ahmed Tinubu

Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 70 anaonekana kati ya wagombeaji wakuu wa tiketi ya urais.

Kiongozi wa kitaifa wa APC, Tinubu alichangia katika uchaguzi wa Buhari mwaka wa 2015.

Tinubu alikuwa gavana wa zamani wa Lagos anayesifiwa kwa kusaidia kukuza maendeleo ya haraka ya mji huo.

Muislamu tajiri wa kusini mwa nchi hiyo, alisema hivi karibuni kwamba kuwa rais wa Nigeria imekuwa ni matarajio ya maisha yote.

Rotimi Amaechi

Hivi majuzi Amaechi alijiuzulu kama waziri wa uchukuzi wa Buhari ili kugombea kwa tikiti ya APC.

Mgombeaji huyo ni mkristo na mwenye umri wa miaka 57 alikuwa gavana wa zamani wa jimbo lenye utajiri wa mafuta la Rivers.

Amekuwa pia spika wa bunge la jimbo na ana mtandao mpana wa mawasiliano na wafuasi kote Nigeria.

Hivi majuzi Amaechi alijiuzulu kama waziri wa uchukuzi wa Buhari ili kugombea kwa tikiti ya APC.

Ahmed Lawan

Lawan ndiye rais wa sasa wa Seneti na mshindani mkuu kutoka kaskazini mwa Nigeria kwa tikiti ya APC.

Kuingia kwake kwenye kinyang’anyiro kumebadilisha mienendo kwani ilidhaniwa kuwa, baada ya uongozi wa Buhari, APC ingetenga tiketi kuelekea kusini kwa Wakristo.

Comments are closed