Search
Close this search box.
Africa

Wizara ya Masuala ya nje inataka bunge kuweka marufuku ya muda kwa Wakenya kuenda Saudia Arabia hadi pale hatua madhubuti za kuwalinda zitakapowekwa.

Akizungumza mbele ya Kamati ya Bunge ya Kazi na Ustawi wa Jamii, Katibu Mkuu Macharia Kamau, anataka marufuku iwekwe kwa wakenya kuajiriwa na kuenda Saudia Arabia.

Bwana Kamau,amesema uamuzi huo umechukuliwa baada ya kuweko na ongezeko la unyanyasaji na vifo vya wakenya wanaofanya kazi Saudia Arabia.

Mwaka wa 2021 pekee wakenya 41 wamepoteza maisha yao na wengine 1,025 wakiwa katika hali mbaya,28 kati ya 41 wakiwa wafanyakazi wa nyumbani. Kamau amesema Wizara ya Kazi inapaswa kuchukua jukumu kuu katika ustawi na usalama wa Wakenya wanaofanya kazi nje ya nchi.

“Hatua za ujasiri na maamuzi bora yanahitaji kuchukuliwa ili kupunguza mateso zaidi kwa Wakenya wanaofanya kazi za nyumbani nchini Saudi Arabia.”Katibu Mkuu Macharia Kamau, amesema.

Katibu Mkuu Macharia Kamau, anasema walijulishwa kuhusu matatizo ya Wakenya baada ya tatizo hilo kukithiri na kama wizara wataweka mikakati ya kuhakikisha Wakenya wanaoishi ughaibuni wanalindwa.

Comments are closed