WAKIMBIZI WA AFGHANISTAN WATAFUTA HIFADHI

“WAKENYA TUMEKUWA WAKARIMU SANA KUWAPA HIFADHI WAKIMBIZI KUTOKA MATAIFA JIRANI AFRIKA, MATAIFA MENGINE YATUSAIDIE SASA” MSEMAJI WA SERIKALI COL.CYRUS OGUNA

MSIMAMO WA SERIKALI YA KENYA KUHUSU KUWAPA HIFADHI WAKIMBIZI

Msemaji wa Serikali ya Kenya Col. Cyrus Oguna

Serikali ya Aghanistan ilitekwa na kundi la Taliban siku 10 tu baada ya serikali kutangaza kuwa itaanza kuondoa majeshi yake nchini humo. Majeshi ya Marekani yamekuwa yakiweka usalama nchini humo kwa miongo miwili. Siku ya Jumapili 15 Agosti , Rais wa Afghanistan, Ashraf Ghani alifaulu kutorokea katika Milki za Kiarabukupata hifadhi baada ya Taliban lufikia mji mkuu wa Kabul

https://youtu.be/jDYICXPE7So

WaAfghanistan wengi walianza kutoroka nchi hiyo baada ya Rais Ghani kutorokea Milki za Kiarabu, umati mkubwa wa watu ulishuhudiwa katika uwanja wa ndege mjini Kabul, wengi waking’ang’anai kupata usafiri.Rais wa Marekani na viongozi wengine kutoka mataifa ya ughaibuni wamefungua mipaka yao na kuwakaribisha wakimbizi kutoka Afghanistan.

Rais wa Marekani na viongozi wengine kutoka mataifa ya ughaibuni wamefungua mipaka yao na kuwakaribisha wakimbizi kutoka Afghanistan.Barani Afrika , Rais wa Uganda Yoweri Museveni alipata agizo rasmi kutoka Ikulu ya Marekani awape hifadhi takriban wakimbizi 2000.Mwanzo TV ilifanya mahojiano ya kipekee na Msemaji wa Serikali nchini Kenya, Col. Cyrus Oguna, kuzungumzia suala la wakimbizi kupata hifadhi Kenya na vile vile suala la kupatikana kwa chanjo zaidi za kukabiliana na UVIKO 19.