Takriban wanawake kumi na wawili waliandamana katika mji mkuu wa Afghanistan siku ya Jumanne kupinga amri mpya ya Taliban kwamba wanawake lazima wafunike nyuso na miili yao kikamilifu wanapokuwa hadharani.
Kiongozi mkuu wa Afghanistan na chifu wa Taliban Hibatullah Akhundzada alitoa agizo mwishoni mwa juma akiwaamuru wanawake kufunika kikamilifu, haswa na burqa ya kitamaduni inayofunika uso wote.
Amri hiyo ilikuwa ya hivi punde zaidi katika msururu wa vikwazo vinavyoendelezwa nchini Afghanistan, ambapo Waislam wamerudisha nyuma mafanikio ya kando yaliyopatikana na wanawake baada ya uvamizi ulioongozwa na Marekani wa kuangusha utawala wa kwanza wa Taliban mwaka 2001.
“Haki, haki!” waliimba waandamanaji, wengi wakiwa na nyuso zisizofunikwa, katikati mwa Kabul. Waandamanaji pia waliimba ‘Burqa sio hijabu yetu!’ wakionyesha pingamizi lao la kutotumia hijab una badala yake kutumia burqa inayoficha uso wote kwa ujumla.
Baada ya msafara mfupi, maandamano hayo yalisitishwa na wapiganaji wa Taliban, ambao pia waliwazuia waandishi wa habari kuripoti tukio hilo.
Amri ya Akhundzada, ambayo pia inawaamuru wanawake ‘kusalia nyumbani’ ikiwa hawana kazi muhimu nje, imezua shutuma za kimataifa.
“Tunataka kuishi kama wanadamu, si kama mnyama fulani aliyefungwa kwenye kona ya nyumba,’ muandamanaji Saira Sama Alimyar alisema kwenye mkutano huo.
Akhundzada pia aliamuru mamlaka kuwafuta kazi wafanyikazi wa serikali wa kike ambao hawafuati kanuni mpya ya mavazi, na kuwasimamisha kazi wafanyikazi wa kiume ikiwa wake na binti zao watakosa kufuata sheria hizo.
Katika kipindi cha miaka 20 ya kutokuwepo kwa uongozi wa miongo miwili ya Taliban madarakani, wanawake walipata mafanikio katika elimu, mahali pa kazi na maisha ya umma lakini mitazamo ya kihafidhina na ya mfumo dume bado ilitawala.
Huko mashambani, wanawake wengi waliendelea kuvaa burqa katika miongo hiyo miwili.
Lakini wasomi na wanaharakati kadhaa wa kidini wanasema mavazi hayo hayana msingi wowote katika Uislamu na badala yake ni kanuni ya mavazi ya Taliban iliyoundwa kuwakandamiza wanawake.
Baada ya kunyakua mamlaka mwaka jana, Taliban walikuwa wameahidi utawala usio mkali wa Kiislamu ambao ulikuwa wa kwanza kutawala kutoka 1996 hadi 2001, lakini vikwazo vingi tayari vimewekwa.
Baadhi ya wanawake wa Afghanistan hapo awali walipinga vizingiti hivyo wakifanya maandamano madogo ambapo walidai haki ya elimu na kazi.
Lakini Taliban hivi karibuni waliwakusanya viongozi hao, wakiwazuia wasijulikane huku wakikana kwamba walikuwa wamezuiliwa.
Tangu kuachiliwa kwao, wengi wamekwenda kimya.