Polisi wa Uganda wamewakamata wanaharakati 21 katika mji mkuu Kampala leo Jumatatu wakati wakipinga mpango tata ya mabilioni ya dola ya mradi wa Mafuta ghafi
Mradi wa Bomba ya Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), unaoongozwa na kampuni kubwa ya mafuta ya Ufaransa ya TotalEnergies, unahusisha kuchimba mafuta nchini Uganda na kupeleka mafuta ghafi Tanzania kwa ajili ya kuuza katika masoko ya kimataifa.
Makundi ya wanaharakati hao yanasema mradi huo una athari mbaya kwa jamii na mazingira wakati uchimbaji unafanyika katika Hifadhi ya Taifa ya Murchison Falls, eneo kubwa zaidi la ulinzi nchini Uganda.
“Kuna watu 21 waliokamatwa, ni pamoja na wanaume 19 na wanawake wawili,” alisema Samuel Wanda, mmoja wa mawakili wa utetezi.
Kundi hilo lilijaribu kuandamana katika bunge na ubalozi wa China huku Nane kati ya wale waliokamatwa wanathiriwa moja kwa moja na mradi wa EACOP
Wakili Samwel wanda Alisema waandamanaji hao walikuwa wakizuiliwa katika kituo kikuu cha polisi mjini Kampala lakini maafisa bado hawajatoa maelezo ya kina kuhusu mashtaka hayo.
Kampuni ya TotalEnergies na China National Offshore Oil Corporation zinachimba visima katika Ziwa Albert, ambalo lina takriban mapipa bilioni 6.5 ya mafuta ghafi, ikiwa ni pamoja na mapipa bilioni 1.4 ambayo kwa sasa yanachukuliwa kuwa yanaweza kutoa faida.
Eacop ni mfumo wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi lenye urefu wa kilomita 1,443 ambao utajengwa kwa ajili ya kusafirisha mafuta ghafi kutoka Wilaya ya Kabaale – Hoima nchini Uganda hadi katika bandari ya Tanga nchini Tanzania.
Bomba hilo litasafirisha mafuta yanayozalishwa kutoka kwenye visima vya mafuta vya Ziwa Albert nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania, ambapo mafuta hayo yatauzwa katika masoko ya kimataifa.