Watu milioni 7 wakabiliwa na uhaba wa chakula Sudan Kusini

Photo courtesy

Takwimu kutoka Umoja wa Mataifa, AU, iliashiria kuwa takriban watu milioni saba kutoka taifa la Sudan Kusini wanakabiliwa na uhaba wa chakula. Idadi hiyo inajumuisha maelfu ya wengine ambao hali yao ya kiafya ni ya kusisitisha mno kwa kuwa wameathirika zaidi

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu imesema kuwa jumla ya watu milioni 9 wanahitaji misaada ya kibinadamu

Uhaba wa chakula katika taifa la Sudan Kusini umechangiwa pakubwa na vita vinavyoendelea katika taifa jiranin la Sudan.

Photo courtesy

Jumla ya watu 670,000, ni raia wa taifa jirani la Sudan, ambao walikimbilia taifa la Sudan Kusini kutokana na vita vinavyoendelea katika taifa hilo. Asilimia 80 kati yao ni raia wa Sudan Kusini, ambao walikuwa wameenda Sudan kutafuta hifadhi.

Takriban miaka 13 baada ya uhuru wake mnamo mwaka 2011, Sudan Kusini ambayo ndio nchi changa zaidi duniani, inakabiliwa na misukosuko ya kisiasa, ghasia na ukosefu wa amani.