Watu watatu wahofiwa kukwama kwenye vifusi vya maporomoko, eneo la Kimende nchini Kenya

Photo courtesy

Watu watatu wanahofiwa kukwama ndani ya vifusi vya maporomoko ya ardhi yaliyotokea Kimende, eneobunge la Lari, Kaunti ya Kiambu, nchini Kenya.

Maporomoko hayo yalitokea Jumanne usiku wakati baadhi ya waathiriwa walikuwa wakielekea nyumbani baada ya shughuli za siku walipofunikwa na vifusi ambayo yanasemekana kusababishwa na mvua kubwa ya mafuriko yaliyonyesha katika eneo hilo.

Juhudi za uokoaji zinaendelea, Jumatano hii, huku kukiwa na hofu kuwa maporomoko hayo yanaweza kuvamia maeneo ya jirani, waki huu mvua ikiendelea kunyesha.

Photo courtesy

Kwa sasa eneo hilo limezingirwa na kutangazwa kuwa eneo hatari, hii ni kulingana na Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya.

Taifa la Kenya limeripoti Jumla ya vifo 289 na zaidi ya watu 280,000 ambao walihama makazi yao baada ya wiki kadhaa za mvua kubwa kunyesha nchini, kwa mujibu wa msemaji wa mserikali wa Kenya, Isaac Mwaura.