Watu wengi wameuawa nchini Nepal kufuatia ajali ya ndege

Ndege iliyokuwa na watu 72 imeanguka karibu na uwanja wa ndege katikati mwa Nepal.

Ndege ya shirika la ndege la Yeti kutoka Kathmandu kuelekea mji wa kitalii wa Pokhara ilianguka na kushika moto.


Mamia ya wanajeshi wa Nepal wanaendelea na operesheni katika eneo la ajali kwenye korongo la mto Seti, kilomita moja na nusu tu kutoka uwanja wa ndege, msemaji wa jeshi aliambia Reuters, akisema ndege hiyo “imevunjika vipande vipande, miili 40 yapatikana”.


Kulikuwa na abiria 68 ndani ya ndege hiyo na wafanyakazi 4 wa ndege hiyo, kati ya abiria hao, abiria 53 ni raia wa Nepali, Wahindi 5, Warusi 4 na Wakorea 2, Ireland 1, Australia 1, Argentina 1 na Ufaransa 1.


Shughuli za uokoaji zinaendelea.