Notice: Function _load_textdomain_just_in_time was called incorrectly. Translation loading for the wordpress-seo domain was triggered too early. This is usually an indicator for some code in the plugin or theme running too early. Translations should be loaded at the init action or later. Please see Debugging in WordPress for more information. (This message was added in version 6.7.0.) in /home/mwanzotv/public_html/wp-includes/functions.php on line 6114
Watu wenye silaha wamewaua watu 32 kaskazini magharibi mwa Nigeria - Mwanzo TV

Watu wenye silaha wamewaua watu 32 kaskazini magharibi mwa Nigeria

Watu wenye silaha waliwauwa watu 32 na kuteketeza makumi ya nyumba katika mashambulizi ya hivi punde zaidi katika jimbo la kaskazini-magharibi mwa Nigeria la Kaduna,mamlaka za mitaa zilisema Alhamisi.

Magenge ya wahalifu waliojihami vikali kutoka kaskazini-magharibi na katikati mwa Nigeria wamevamia vijiji ili kuwateka nyara au kuua wakaazi kwa miaka mingi lakini wamezidisha mashambulizi hayo katika siku za hivi karibuni..

Katika miezi ya hivi karibuni, wameshambulia treni ya abiria kati ya mji mkuu wa Abuja na mji wa Kaduna na kuwateka nyara makumi ya watu na kuua zaidi ya wanavijiji 100 na makumi wengine wanachama wa vikundi vya kuweka usalama.

Siku ya Jumapili, “majambazi walishambulia vijiji vya Dogon Noma, Ungwan Sarki na Ungwan Maikori katika eneo la serikali ya mitaa ya Kajuru,” kamishna wa usalama wa serikali Samuel Aruwan alisema katika taarifa.

Alisema “walivamia eneo hilo kwa wingi wakiwa na pikipiki, na kupora nyumba kadhaa, huku wakiwavamia na kuwaua wenyeji.”

Watu hao wenye silaha walishambulia maeneo mawili ya kwanza na kuwaua raia 31.

“Baadaye walielekea Ungwan Maikori, ambapo walimuua mtu mmoja na kuchoma baadhi ya nyumba,” alisema Aruwan.

Vikosi vya usalama vilituma helikopta ambayo iliwakabili majambazi.

Kwa mujibu wa Mradi wa Armed Conflict Location and Event Data Mradi wa Data (ACLED), majambazi hao wenye silaha waliua raia 2,600 mwaka wa 2021, ongezeko la asilimia 250 kutoka 2020. Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, jenerali wa zamani wa jeshi, amekuwa chini ya shinikizo kukomesha ghasia mbaya kabla ya kuondoka madarakani mwaka ujao mwishoni mwa mihula yake miwili madarakani.