Search
Close this search box.
Africa
Nigel Mullinder mwanachama wa The Upsidedown kwenye chumba lililotengwa nchini Afrika Kusini.

Muda mfupi baada ya usiku kuingia, Rivas Bright akiwa akiwa amebeba tochi mkononi, anagonga mara mbili kwenye dirisha lililovunjika la jengo lililotelekezwa mjini Pretoria Afrika Kusini.

“Bado! Anawaambia wawindaji mizimu wenzake. Washikilia pumzi zao, wakisubiri majibu kutoka kwa vivuli.

Ni takriban miaka miwili tangu Bright, mwenye umri wa miaka 39 aanzishe kikundi cha The Upsidedown ambacho kinajumuisha wakereketwa wa hali ya juu ya wawindaji mizimu katika harakati za kuthibitisha uhalisia wa mizimu.

Kazi yenyewe ni nzito. Kwa kuwa roho za mizimu hukwepa mashambulia au muingiliano wa aina yeyote.

Nigel Mullinder mwenye umri wa miaka 29 ni mwanachama wa kikosi hicho ambaye mchana anafanya kazi kwenye kampuni ya uchezaji Kamari (Casino), anasema masomo kuhusu matukio yasiyo ya kawaida yamewavutia watafiti na wanasaikolojia ila juhudi zao zimetoa ushahidi mdogo mno.

Bright na kikosi chake cha wasioamini uwepo na masuala ya mizimu kinachojumuisha wanaume watano na wanawake wawili, sasa wamegeukia teknolojia ili kutatua fumbo hilo.

Wakiwa wamejihami na zana nyingi ikiwa pamoja na kamera, vitambua mwendo na joto, redio na programu ya kufichua shughuli zisizo za kawaida, wanakagua  majengo yaliotengwa wakitafuta vidokezo katika mapango na ngazi zenye kutu.

“Tunahitaji ushahidi ambao utaturuhusu kuthibitisha kwamba sio tu upepo unaovuma kupitia dirishani au mlango unaofungwa kwa sababu ya aina fulani za mitikisiko,” ansema Mullinder.

Usiku wa kuamkia leo wamefika kwenye jengo lililotelekezwa ndani ya ndaki ya chuo kikuu kimoja kikubwa Afrika Kusini, ambalo liliomba lisitajwe kwa jina.

Walinzi wa usiku wametishwa ya kutishwa na kelele za kutisha.

Lucy Tsoeu anasema milango inayogonga, kugonga kwa mashine yakupiga chapa usiku kumemfanya aamini uwepo wa mizimu chumbani.

Mfanyikazi mwenzake Mpho Mthombeni naye anasema amesikia vyoo vikiwa na maji na kuhisi uwepo wa ajabu wakati hakuna lolote.

“Nifanye nini jamani? Je! Niomba, au nitasema kwa sauti zaidi ili kuwatisha?” anashangaa Tsoeu.

-Vivuli, minong’ono na milio ya risasi-

Akiwa amevalia shati tao la kijivu na suruali nyeusi, Bright ambaye ni mfanyikazi wa duka la reje reja, anasema ameskia sauti za kutisha na kuona vivuli vibaya tangu akiwa na umri mchanga sana.

“Mamangu angedai kuzungumza na mizimu jikoni kwake,” anasema Bright.

Tangu alipoanzisha kikundi hicho cha “The Upsidedown” wamejikusanyia wafuasi elfu chache kwenye mitandao ya kijamii,kutumia maelfu ya dola kununua vifaa na kutafuta takriban majengo kadhaa, kufuatia vidokezo kutoka kwa wenyeji waliokuwa na wasiwasi.

Katika jengo la chuo kikuu kikundi hicho hukagua kila chumba na kuweka zana zao za kugungua matukio kwenye sakafu iliyofunikwa na matawi ya mimea yaliokauka.

“Kwa kweli sisi ni kundi la wavulana ambao husimama gizani, kuuliza maswali na kufuata taa nyekundu na kijani zinazowaka,” anasisitiza Bright.

Kundi hilo, linalojumuisha wanzungu, waafrika Kusini wa tabaka la kati limekuwa kwenye jengo hili kabla ya mwezi mmoja uliopita.

Kisha, wanachama wake wanasema waliwasiliana na mizimu ya watoto katika chumba ambacho kilitumika kama chumba cha kuhifadhi maiti cha muda wakati wa ghasia kali miaka ya 1980.

Mullinder anajaribu kuwasiliana tena, akisiliza mita ya masafa ya redio akiwa amefumba macho.

Kila kitu kinarekodiwa ili kunasa ushahidi unaowezekana. Lakini matokeo bado hayajakamilika.

Comments are closed