Huku ikiwa maabara pekee yakuzalisha chanjo iliyoidhinishwa dhidi ya monkeypox, kampuni ya Denmark ya Bavarian Nordic imeshuhudia ongezeko la uagizaji wa chanjo hiyo huku ugonjwa huo ukienea kote ulimwenguni.
“Idhini tuliyopata mwaka wa 2019, tulipouza labda dozi mia chache tu, ghafla ikawa muhimu sana kwa afya ya kimataifa,” makamu wa rais wa kampuni hiyo Rolf Sass Sorensen anasema huku akitabasamu katika makao makuu ya kampuni ya kibayoteki huko Copenhagen.”
Bavarian Nordic ilipata mshangao baada ya kuenea kwa ghafla kwa ugonjwa huo mapema mwaka huu katika nchi kadhaa nje ya Afrika Magharibi na Kati.
Lakini Sorensen anasema ana imani kuwa kampuni hiyo inaweza kukidhi mahitaji ya kimataifa ingawa ina kituo kimoja tu cha uzalishaji.
“Kwa mahitaji ya sasa tunaweza kusambaza kwa soko la kimataifa kwa urahisi. Tuna dozi milioni kadhaa kwa wingi ambazo zitahakikisha kuwa mlipuko wa sasa unashughulikiwa,” aliiambia AFP
Bavarian Nordic ina uwezo wa uzalishaji wa kila mwaka wa dozi milioni 30 za chanjo.
Chanjo ya ndui iliyozalishwa na kampuni ya Denmark, inayouzwa kama Imvanex barani Ulaya, Jynneos nchini Marekani na Imvamune nchini Canada, ni seramu ya kizazi cha tatu (chanjo hai ambayo haijirudii katika mwili wa binadamu).
Imepewa leseni barani Ulaya tangu 2013. Iliundwa dhidi ya ndui kwa watu wazima, ugonjwa unaozingatiwa kutokomezwa miaka 40 iliyopita, na inahitaji dozi mbili kwa chanjo.
Kulingana na Sorensen, chanjo hiyo inapatikana ‘katika nchi nyingi’ na inaweza pia kutumika dhidi ya monkeypox, kabla na baada ya kuambukizwa virusi.
“Ukichanjwa siku chache baada ya kuambukizwa, unaweza pia kulpata kinga,”alifafanua.
Baada ya kupata ruhusa kutoka kwa Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Marekani (FDA) miaka mitatu iliyopita kutumia chanjo yake ya ndui dhidi ya monkeypox, Bavarian Nordic sasa inatuma ombi la kufanya hivyo barani Ulaya.
Mamlaka yaThe European Health Emergency Preparedness and Response Authority (HERA), iliyoundwa na Tume ya Ulaya wakati wa janga la Covid-19, tayari imenunua zaidi ya dozi 100,000 kwa nchi 27 za EU na vile vile Norway na Iceland.
Uwasilishaji wa kwanza unatarajiwa mwishoni mwa Juni kwa nchi hizo ambazo zinazingatiwa kuwa kipaumbele.