Waziri Mkuu Majaliwa Ampa Naibu Wake Siku Saba Kutatua changamoto ya uhaba wa mafuta

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amemuagiza Naibu wake, Dotto Biteko, kutafuta muarobaini wa changamoto ya uhaba wa mafuta ndani ya siku saba.

Hii inakuja wakati ambapo katika baadhi ya maeneo nchini Tanzania kumekuwa na uhaba wa mafuta katika baadhi ya maeneo hatua iliyofikia baadhi ya watu kupanga foleni kwenye vituo vya mafuta
Wakati bei za mafuta ya Petrol, Dizel na mafuta ya taa zikiendelea kuongezeka bado upatikamnaji wake katika baadhi ya mikoa nchini Tanzania umekuwa ni mgumu huku sababu mbalimbali zikitajwa ikiwemo baadhi ya wanunuzi wa mafuta wakidaiwa kuficha bidhaa hiyo.

Hii leo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Naibu Wazir Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati, Dotto Biteko kutafuta suluhu ya jambo hilo lililozua sintofahamu na mamlalamiko kutoka kwa watumiaji.

Katika agizo lake hilo, Waziri Majaliwa amemtataka  Biteko kufanya kikao na taasisi zinazoshughulika na biashara ya mafuta, pamoja na wafanyabiashara, kuona namna ya kupanua wigo wa uagizaji wake, ili nchi iwe na akiba ya kutosha.

“Ili watanzania wapate huduma hiyo muhimu ya upatikanaji wa mafuta, wanunuaji na taasisi ya uuzaji wa mafuta mtengeneze kikao kikubwa na wizara zinazohusika. Mkae muone namna ya upatikanaji wa mafuta.
“Tupanue wigo wa waagizaji mafuta ili tuwe na mafuta mengi nchini kwa usalama wa taifa letu na kama hii itafanyika ndani ya wiki moja tutakuwa tumepata majibu na tutawapa taarifa watanzania na naibu waziri mkuu atashughulikia hilo,” amesema Majaliwa.

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji nchini Tanzania (EWURA) Septemba 4,2023  ilisema bado kuna akiba ya kutosha ya mafuta inayotosheleza kwa siku 19 ikimaanisha kwamba nchi ina mafuta ya kutosha zaidi ya mahitaji ya sheria ya petroli inayotaa maghala muda wote yawe na mafuta ya siku 15.

Hata hivyo Spika wa bunge Dkt Tulia Akson amesema ni wakati sasa wa kufanya tathimini maalum ya mfumo unaotumika kuagiza mafuta kwa pamoja ili kuona ni sababu zipi zinasababisha uwepo wa changamoto ya upatikanaji wa bidhaa hiyo

Aidha, Waziri Majaliwa amesema Biteko ameshaanza kufanya vikao kadhaa na wadau kwa ajili ya kutafuta suluhu ya changamoto hiyo, iliyokuwepo tangu January Makamba, alivyokuwa Waziri wa Nishati.

“Kufuatia mabadiliko ya Rais Samia Suluhu Hassa aliyoyafanya juzi, tumeanza kumuona naibu waziri mkuu akifanya vikao kadhaa na wizara na kukutana na wadau. Kwa kuwa ameshaanza hii kazi niendelee kumuagiza kushughulikia suala hili zaidi mafuta yapatikane nchini, suala la bei tunajua zinabadilika wakati wote,” amesema Waziri Majaliwa.