Waziri wa mambo ya ndani wa Ukraine na watu 15 wafariki katika ajali ya Helikopta

 

Waziri wa mambo ya ndani wa Ukraine ni miongoni mwa watu 18 waliuawa baada ya helokopta kuanguka kando ya shule ya chekechea karibu na mji mkuu  Kyiv.

Watoto watatu pia walikuwa miongoni mwa waliofariki na wengine 15 wanaendelea kupokea matibabu hospitalini.

Waziri huyo Denys Monastyrskiy alikuwa na watu wengine wanane kwenye helikopta hiyo.

Katika video ambao ilisambaa mitandaoni baada ya ajali hiyo, milio iliskika katika eneo la mkasa ambayo iliteketezwa na moto.

Mabaki ya helikopta yalikuwa nje ya jengo linalowaka moto.

Moto ulizuka karibu na shule ya chekechea na watoto na wafanyikazi walihamishwa kutoka kwa jengo hilo.

Kulikuwa na giza na ukungu wakati wa ajali hiyo na ripoti za awali zinasema helikopta hiyo iligonga shule ya chekechea kabla ya kuanguka karibu na jengo la makazi.

Hakujakuwa na taarifa kamili kuhusu chanzo cha ajali hiyo hadi kufikia sasa.

“Kwa ujumla watu 18 wamejulikana kupoteza maisha yao,” mkuu wa polisi wa kitaifa Igor Klymenko amesema.

Kati ya walioaga ni maafisa wakuu wa wizara ya mambo ya ndani wakiwemo waziri Denys Monastyrsky na naibu wake Yevgeniy Yenin.

Monastyrdky mwenye umri wa miaka 42 na ambaye alikuwa baba ya watoto wawili, aliteuliwa kuwa waziri wa mambo ya ndani mwaka wa 2021.

Watu 20 wako hospitalini wakiwemo watoto 10.

Maafisa wamesema kwamba wa mkasa watoto na wafanyikazi walikuwepo katika shule hiyo ya chekechea.

Eneo la mkasa mjini Brovary inapatikana kilomita 20 kaskazini mwa Kyiv.

Maafisa wa usalama wa Russia na Ukraine walipigana kuteka mji huo wa Brovary wakati wa mwanzo wa uvamizi wa Moscow hadi vikosi vya Russia vikaondoka mapema mwezi aprili. Rais wa Russia Vladimir Putin alituma vikosi vyake  katika taifa la Ukraine linalounga mkono magharibi februari mwaka uliopita.

Ajali hiyo inajiri wakati kuna janga ambalo lilipelekea watu 45 miongoni mwao watoto sita kuaga dunia wakati bomu ya Russia ililipukia katika jumba la makaazi mashariki mwa mji wa Dnipro wikendi iliyopita.