WHO: Janga la UVIKO- 19 halijaisha na ulimwengu unapaswa kutarajia “aina hatari zaidi ya virusi” kuibuka

Tedros Adhanom Ghebreyesus, Mkurugenzi Mkuu WHO

Shirika la Afya Duniani mnamo Ijumaa lilionya kwamba janga la UVIKO-19 bado halijaisha na kusema kuna uwezekano wa kirusi kipya.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus aliwaambia waliohudhuria Mkutano wa Usalama wa Munich nchini Ujerumani kwamba chanjo na ukweli kwamba Omicron imegeuka kuwa kirusi kisicho kikali sana “imefanya watu wengi kuwa na dhana kwamba janga hilo limekwisha.”

“Lakini sivyo.” maanake watu 70,000 kwa wiki wanakufa kutokana na ugonjwa unaoweza kuzuilika na unaotibika,” Ghebreyesus aliongeza.

“UVIKO 19 bado ni hatari ikiwa “83% ya wakazi wa Afrika bado hawajapokea dozi ya kwanza ya chanjo,” aliendelea.

 “Bado ni hatari ikiwa mifumo ya afya inaendelea kushindwa na kukabiliana na ugonjwa huu.”

Wakati bado wa kusheherekea ikiwa bado tuna virusi vinavyoambukiza sana vinavyoenea bila kudhibitiwa, na kuna ufuatiliaji mdogo sana wa virusi vipya vinavyoweza kuibuka,”Ghebreyesus pia alionya kwamba ulimwengu unapaswa kujiandaa kwa uwezekano wa virusi zaidi kutokea. Kwa kweli, hali ilivyo kwa sasa watu zaidi huenda wakaambukizwa. virusi hatari zaidi vitaibuka,” alisema.