WHO Latangaza Virusi vya MPOX kuwa Dharura ya Afya Duniani

Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani, WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus, ametangaza virusi vya Mpox kuwa ni dharura ya afya ya umma duniani kutokana na kuongezeka kwa maambukizi yake barani Afrika.
Muathiriwa wa virusi vya MPOX barani Afrika
Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani, WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus, ametangaza virusi vya Mpox kuwa ni dharura ya afya ya umma duniani kutokana na kuongezeka kwa maambukizi yake barani Afrika.
Mkurugenzi huyo ametangaza hatua hiyo baada ya mkutano na kamati ya dharura ya shirika hilo la afya la Umoja wa Mataifa.
Ripoti kutoka WHO, linasema kuwa zaidi ya watu 14,000 wameambukizwa virusi vya mpox hadi sasa katika mwaka huu huko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na wengine wapatao 524 wameshakufa.
Children with lesions, one of the symptoms of Monkey Pox, during an outbreak in the north of the country. Monkeypox is a viral disease, related to smallpox. It can be transmitted from animals to humans, usually via contact with infected bushmeat or by being bitten or scratched by an infected animal. Human to human transmission can occur via respitory droplets (requiring prolonged face-to-face contact). The disease is usually found in central and west Africa although the central African strain is more likely to be fatal with about 10 to 15 percent of infected people dying from Monkeypox. *** Local Caption ***
africa health disease children
Shirika la Afya la Umoja wa Afrika lilitangaza hali ya dharura ya afya ya umma siku ya Jumanne kutokana na mlipuko wa ugonjwa huo wa Homa ya Nyani unaoongezeka katika bara LA Afrika, likisema hatua hiyo ni wito wa wazi kwa mamlaka zote kuchukua hatua.
Mkuu wa Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa barani Afrika, CDC, Jean Kaseya ameeleza kuwa kirusi cha Mpox kwa sasa kimevuka mipaka katika kusambaa kwake na kimewaathiri maelfu ya watu katika barani Afrika.
Wataalamu wakimuuguza mtoto anayeshukiwa kuambukizwa virusi vya MPOX
Wanasayansi kwa upande wao wameelezea wasiwasi wao juu ya kuenea kwa aina mpya ya ugonjwa ambao watu wanaweza kuambukizana kirahisi.
Mpox (Homa ya Nyani), iligundulika hivi karibuni kwa mara ya kwanza katika nchi nne za Afrika Mashariki ambazo ni Burundi, Kenya, Rwanda na Uganda.
Gebreyesus amesema kuna wasiwasi wa kuenea zaidi kwa maambukizi ya mpox barani Afrika na kwingineko duniani
duniani.
 
Vyanzo: AP/AFP