TCRA yatoa sababu ya kuitoza faini Zama Mpya Tv
Akizungumza na waandishi wa habari leo Dar es Salaam, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Habi Gunze, alisema Agosti 12, mwaka huu, TCRA ilitoa leseni kwa Zama Mpya Tv na Agosti 28 mwaka huu walichapisha taarifa za uchochezi kuhusu tozo za serikali kwenye ukurasa wa twitter kinyume na kanuni ya 9 (a), 12 (a) (I) na 16 (1) aya 3 (a), (d), (g), (h) na (k) ya kanuni za kielektroniki na Posta ya mwaka 2020.