Mdude agoma kutoa simu kwa ajili ya uchunguzi polisi, ataka zichukuliwe kwa amri ya Mahakama.
Mwanaharakati na kada wa CHADEMA Mdude Nyagali ameijibu barua ya Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai mkoani Mbeya, iliyomtaka kukabidhi simu zake na vifaa vingine vya kielektroniki kwa ajili ya kufanyia uchunguzi kuhusiana na kauli na machapisho aliyoyatoa mnamo tarehe 9 Julai,2023.