14 kizimbani kwa tuhuma za utakatishaji fedha zaidi shilingi milioni 350.
Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa Takukuru Mkoani Mbeya imewafikisha mahakamani watu 14 wakiwemo watumishi wa Halmashauri mbalimbali mkoani humo wakituhumiwa kwa makosa 16 ikiwemo kuendesha genge la uhalifu na utakatishaji wa fedha zaidi ya shilingi Million 350.