Madaktari Muhimbili wamtoa mtoto kipande cha plastiki kwenye mapafu alichoishi nacho miezi 23
Madaktari Bingwa wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wamefanikiwa kutoa kipande cha plastiki kwenye pafu la kushoto la mtoto mwenye umri wa miaka 11, kupitia kifaa maalumu kinachoitwa Flexible Bronchoscopy.