Lissu atumia saa 7 kumuhoji shahidi wa Jamhuri katika kesi ya uhaini
Katika mahojiano hayo, Lissu alitumia takribani saa saba kumuhoji Shahidi huyo kuanzia majira ya saa 3:30 mpaka saa 10, muda wote aliutumia kupima uhalali wa ushahidi wa shahidi huyo, akihusisha masuala mbalimbali kulinga na ushahidi aliouandika katika maelezo yake ikiwamo ya taratibu za kiuchunguzi, matumizi ya notebook ya polisi, video za ushahidi na tafsiri ya maneno yaliyotumika kwenye mashtaka ya uhaini.