Lissu apinga vielelezo vya ushahidi wa video kupokelewa Mahakamani
Lissu aliwasilisha hoja zake baada ya shahidi wa tatu wa upande wa Jamhuri kuendelea kutoa ushahidi wake kwa siku ya pili mfululizo, akihojiwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Thawabu Issa kuhusu uchunguzi wa kitaalamu alioufanya kwenye video inayodaiwa kumhusu Lissu.