Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) nchini Kenya imemtangaza William Ruto kuwa mshindi wa kiti cha Urais baada ya kupata asilimia 50.49 huku akimshinda mpinzani wake Raila Odinga aliyepata kura asilimia 48.85
Baada ya Tume ya Uchaguzi kumtangaza William Ruto kuwa mshindi wa kiti cha Urais, sasa mteule huyo anatarajiwa kuapishwa baada ya siku 14 ambapo atapokea kijiti cha uongozi wakati ambapo nchi ina hali mbaya ya kiuchumi
Itakumbukwa waliowania kinyang’anyiro cha kiti cha urais walikua wagombea wanne ambao hadi muda huu matokeo yanatangazwa matokeo yamesomekaWilliam Ruto 50.49%
Raila Odinga 48.8%
Waihiga Mwaure 0.23%
Wajackoyah George 0.44%
Ruto ndiye mshindi wa kiti cha Urais.