Wabunge tisa kuiwakilisha Tanzania bunge la Afrika Mashariki.

Wabunge hao wamechaguliwa leo Alhamisi, Septemba 22, 2022 bungeni jijini Dodoma.

0

Bunge la Tanzania limewachagua wabunge tisa watakaoiwakilisha nchi hiyo katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (Eala).

Kati ya wabunge hao tisa, mmoja ni wa upinzani kutoka Chama Cha Wananchi (CUF) ambaye ni Mashaka Ngole.

Wabunge hao wamechaguliwa leo Alhamisi, Septemba 22, 2022 bungeni jijini Dodoma.

Spika wa Bunge la Tanzania, Dk Tulia Ackson amewatangaza waliopitishwa ni Angela Kizigha, Dk Shogo Mlozi, Nadra Mohammed, Dk Abdullah Makame, Machano Machano, Ansari Kachwamba, James Millya na Dk Ng’waru Maghembe ambao wote ni wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Miongoni mwa wagombea walioangukia pua kwenye kinyang’anyiro hicho ni Ado Shaibu ambaye ni Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo akizidiwa kura na Mashaka wote kutoka vyama vichache vyenye uwakilishi Bungeni kati ya

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted