Kesi ya Maofisa wa polisi wanaodaiwa kumuua mfanyabiashara wa madini kusikilizwa kesho.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mtwara imepanga kusikiliza tena kesi ya mauaji inayowakabili maofisa saba wa polisi mkoani Mtwara wanaodaiwa kuhusika na mauaji ya mfanyabiashara wa madini, Mussa Hamisi (25) mkazi wa Kijiji cha Ruponda, wilayani Nachingwea mkoani Lindi.

Mara ya kwanza maofisa hao walifikishwa mahakamani Januari 25, mwaka 2022 kwa tuhuma za kufanya mauaji ya hayo ambayo yalizua hisia mseto na kuleta taswira mbaya kwa jeshi la polisi nchini Tanzania

Kesi hiyo ni namba 01 ya Mauaji mwaka 2020/2022 ambapo inadaiwa kuwa Januari 5 mwaka 2022 maofisa hao wa polisi walimuua Musa Hamis (25), mkazi wa Nachingwea mkoani Mtwara baada ya kumpora shilingi  milioni 70.

https://mwanzotv.com/2022/02/22/kesi-ya-maofisa-saba-wa-polisi-wanaodaiwa-kuua-yapigwa-tena-kalenda/

Washtakiwa wanaohusishwa na mauaji hayo ni ofisa Upelelezi (OC CID) Wilaya ya Mtwara, Gilbert Kalanje, Mkuu wa Kituo cha Polisi Mtwara (OCS), Charles Onyango, Ofisa wa Intelijensia ya Jinai Mkoa wa Mtwara, Charles Kisinza na Mkaguzi wa Polisi, John Msuya pamoja na Mganga Mkuu wa Zahanati ya Polisi, Marco Mbuta. 

Wengine ni Mkaguzi wa Polisi, Shirazi Mkupa na Koplo Salimu Juma Mbalu.

https://mwanzotv.com/2022/02/08/kesi-ya-maofisa-wa-polisi-yapigwa-kalenda/