Watu 10 wamethibitishwa kufariki kufuatia shambulio katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.
Mamlaka inasema jengo wamemaliza hali ya kuzingirwa kwa jengo lililokuwa likishambuliwa na wapiganaji wa kundi la kiislamu la al-Shabab.
Wapiganaji wa kundi hilo waliokuwa na silaha nzito walivamia jengo linalokaliwa na wanamgambo wanaoiunga mkono serikali Jumanne usiku na kuua watu kadhaa.
Ilichukua masaa kwa mamlaka kumaliza kuzingirwa katika wilaya ya AbdiAziz.
Milio ya risasi na milipuko mikali ilisikika hadi Jumanne usiku. Vikosi vya usalama vinasema waliwaua wanachama wanne wa al-Shabab, ambao walidai kutekeleza shambulio hilo.
Kundi hilo limepoteza maeneo makubwa katika miezi ya hivi karibuni kufuatia mashambulizi ya jeshi la Somalia linaloungwa mkono na Umoja wa Afrika na vikosi vya Marekani, na wanamgambo wa koo.
Lakini mashambulizi kama haya katika moyo wa mji mkuu yanaonyesha bado ni tishio kuu kwa serikali ya shirikisho.