Rais wa Kenya William Ruto ameiomba Afrika kufanya juhudi za pamoja ili kushinda vita dhidi ya mabadiliko ya hali ya anga.
Ruto ameseam bara afrika limeathiriwa kwa kiasi kikubwa na athari zake mbaya.
Alibainisha kuwa urekebishaji upya wa kitaasisi na uwekaji upya wa kiuchumi unaotokana na mabadiliko haya, utaiweka Afrika kama taifa lenye nguvu kubwa ya kiuchumi duniani.
Alikuwa akizungumza Jumatatu wakati wa Kongamano la 3 la Kikanda la majaji Barani Afrika katika Hoteli moja Kaunti ya Nairobi.
Rais alisema changamoto inayo ambatana na hali ya hewa yanayokuja ni ya kutisha sana kwa Afrika, hususna wakati Afrika ikokwenye kipidi cha amani na ustawi.
Aliuambia mkutano huo kuwa licha ya ukweli kwamba Afrika imejikita katika kukabiliana na umaskini na ukosefu wa usawa, njia ya uchafuzi wa mazingira sio chaguo.
Aliipongeza Idara ya Mahakama kwa kuchukua nafasi ya mbele katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya anga.
Kongamao hilo lilihudhuriwa na majaji wakuu kutoka mataifa yote ya Afrika