Wanachama wa CUF wazidi kutimka

Aliyekuwa Mwenyekiiti wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama Cha Wananchi CUF ambaye pia aliwahi kuwa Mbunge wa Viti Maalum katika Bunge la la 10, Kiza Mayeye amejiondoa kwenye...

0

Aliyekuwa Mwenyekiiti wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama Cha Wananchi CUF ambaye pia aliwahi kuwa Mbunge wa Viti Maalum katika Bunge la la 10, Kiza Mayeye amejiondoa kwenye Chama hicho na kujiunga na Chama cha ACT Wazalendo.

Mayeye amesema kuwa pamoja na na kuchukua uamuzi huo pia ameshajiandikisha katika mfumo wa chama hicho wa kieletroniki.

“Leo, nimelazimika kuchukua maamuzi haya magumu kwa sababu ambazo haziwezi kuzuilika. Mosi, mimi ni mwanasiasa wa vitendo. Naamini siasa halisi ipo chini (field), kwa wananchi. Mwaka 2020 niligombea Ubunge katika Jimbo la Kigoma Kaskazini na kwa matokeo halisi nilishinda lakini  kilichotokea mwaka 2020 sote tunakifahamu,” amesema Mayeye

Kutokana na hali hiyo amesema kuwa mwaka 2020 walioshinda walishindwishwa na walioshindwa walishindishwa!

Amesema Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilipotangaza kuwa amekuwa mshindi wa pili kwa kupata kura 16,252 kila mmoja alishangaa

“Bila shaka hata CCM wenyewe walishangaa, kwa sababu walijua nilishinda!. Ninajiunga ACT Wazalendo ili kuendeleza mapambano. Nimefanya uchambuzi wa kina na kujiridhisha kuwa ACT Wazalendo ndio jahazi sahihi la kuendeleza harakati zangu kwa ajili ya kuwakomboa wanachi wa Kigoma Kaskazini, Mkoa mzima wa Kigoma na Tanzania kwa ujumla.

“Nimevutiwa sana na sera za ACT Wazalendo za kujenga Tanzania ya wote kwa maslahi ya wote. Nimeshawishika pia na jitihada za Chama kuimarisha mtandao wake nchi nzima. Nimevutiwa pia na jitihada za Chama kukuza vipaji vya vijana na wanawake,” amesema

Kiongozi huyo amesema kuwa kabla hajafanya uamuzi huo alizungumza na vyama vingi ili kufanya utafiti kabla ya kujiunga na chama husika.

“Mwishowe nikafanya hitimisho kuwa ACT Wazalendo ndio jukwaa sahihi. Wale ambao walitarajia nitajiunga nao, waniwie radhi, vigezo vya kisayansi vimenipeleka ACT Wazalendo.

“Nimekuja kuongeza nguvu kwenye ujenzi wa Chama katika kujihakikishia ushindi kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025. Ninatarajia kwenda Jimboni Kigoma Kaskazini hivi karibuni, huko nitaeleza kwa kina zaidi kwa nini chama hiki kinapaswa kuwa tumaini lao kutokana na utafiti na uchambuzi wa kina nilioufanya,” amesema

.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted