Pombe yakatisha maisha ya Zahara, mwimbaji wa Afrika Kusini

Nchini Afrika Kusini anajulikana kama Bulelwa Mkutukana, lakini dunia inamtambua kama Zahara. Mmoja wa wanamuziki wa kike wa Afrika Kusini waliofanikiwa kuiteka dunia na hisia za wapenda muziki.

Amejikusanyia mashabiki wengi duniani kutokana na kipaji chake na uwezo mkubwa wa kutuliza hisia za mashabiki.

Kifo kimakatisha sauti ya Zahara

Mwimbaji huyo mashughuli aliyeshinda tuzo myimgi alifariki Jumatatu usiku kutokana na tatizo la Ini lililotokana na unywaji wa pombe kupita kiasi.

Alikuwa amelazwa katika hospitali ya Johannesburg.

Mnamo Novemba, familia ya Zahara ilithibitisha kuwa alikuwa amelazwa hospitalini.

Waziri wa Michezo, Sanaa na Utamaduni wa nchi hiyo, Zizi Kodwa, amesema Serikali imekuwa na familia kwa muda sasa” huku akielezea masikitiko yake kuhusu kifo cha mwimbaji huyo.

Zahara, ambaye kufikia sasa ametoa albamu tano, alitajwa kuwa kwenye orodha ya Wanawake 100 ya BBC mwaka wa 202o. Pia alishinda tuzo kadhaa na kutambuliwa.

Mnamo 2019 Zahara aliweka bayana kuwa alikuwa anapambana na uraibu wa pombe.

Hata hivyo, hadi wakati wa kuwasilisha hili, familia bado haijatoa taarifa yoyote.

Zahara alijulikana kwa gitaa lake la biashara na mtindo wa nywele mkubwa wa Afro. Aliingia kwenye ulingo wa muziki mwaka wa 2011 baada ya albamu yake ya kwanza Loliwe kuuzwa katika muda wa saa 72. 

Umahiri wake wa kuimba kwa hisia na suati yenye kupanda na kushuka, iliwafanya baadhi ya mashabiki wa muziki kumuona kama mrithi sahihi wa Brenda Fassie kwa Afrika Kusini.

Zahara alizaliwa Novemba 9, mwaka 1987 na kama ilivyo kwa wasanii wengine duniani, kipaji chake kilianza kuonekana akiwa bado binti mdogo. Albamu yake ya kwanza ya Loliwe akiwa chini ya lebo ya TS Records ilitoka mwaka 2011. Hata hivyo, miaka kadhaa baadaye ilikuja kuwa maarufu zaidi na hapo akajulikana kila kona.

Pia, ana albamu ya Phendula iliyotoka mwaka 2012 yenye nyimbo za Impilo, Stay na Phendula yenyewe. Mwaka 2015 aliachia albamu yake ya tatu ya Country Girl na hapo akaachana na TS Records na kuwa chini ya Warner Music alikovuna fedha nyingi zaidi.

Akiwa na Warner alirekodi albamu za Mgodi mwaka 2017 na Ngaba Yam ya mwaka 2021 ikiwa albamu yake ya tano na ya mwisho.

Enzi zake za uhai Zahara ameshinda tuzo 17 tofauti na amewahi kuwa Jaji wa Shindano la Idols Afrika Kusini