Azimio yagawanyika kuhusu mdahalo baina ya Upinzani na Serikali

Rais william Ruto siku ya Ijuma amefanya uteuzi wa baraza lake la mawazi ambapo amewateuwa mawaziri 11 kati ya 22 wanaohitajika kikatiba. Ruto amesema mawaziri 11 waliosalia watatangazwa hivi karibuni baada ya kufanaya mazungunzo na upinzani.

hata hivyo mgawanyiko mkubwa katika Muungano wa upinzani kenya umeshuhudiwa   ambapo baadhi ya viongozi wamepinga kufanyika kwa mazngumzo yeyote yatakayopelekea baadhi ya viongozi wao kuorodheshwa katika baraza la mawaziri.

Kinara wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka ambaye ni mmoja wa viongozi wa Upinzani kenya alipinga mpango wowote wa kuwajumuisha viongozi wa upinzani katika serikali hiyo ya Muungano.

Hata hivyo Chama cha ODM kinachoongozwa na Raila Odinga kikionekana kuunga mkono mazungumzo ya kuunda serikali ya Umoja Kenya