Mwanamuziki Wa Wimbo Wa “Rafiki Pesa” Afariki Dunia

 

Shari Martin

Msanii nguli nchini Kenya, Shari Martin, aliyejulikana sana kwa wimbo wake wa “Rafiki Pesa,” amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 54.

Shari Martin alifariki Agosti 2, 2024, akipokea matibabu katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta kutokana homa ya mapafu (nimonia).

Shari Martin

Taarifa hiyo ya tanzia ilitolewa hii leo Jumanne, Agosti 6, 2024, na mwanamuziki, Douglas Jiveti, kupitia mtandao wake wa Kijamii, na kuthibitishwa na rafiki wake wa karibu wa kike na ambaye vilevile ni msani, aliyejitambulisha kwa jina moja, Pauline .

“Mwanamuziki wa Injili wa Pioneer Shari Martin amefariki dunia kwa huzuni. Mwanamuziki mwenye vipawa sana: mtunzi wa ubunifu, nyimbo kali, sauti nzuri. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi,” alisema Douglas.

Shari Martin atakumbukwaa sana kutokana na muziki wake wa “Rafiki Pesa,” ambao umeacha athari kubwa kwa wengi.