Rais Samia Atii amri ya Wamaasai, aagiza huduma zote zirejeshwe Ngorongoro

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametii amri ya Jamii ya wamaasai taarafa ya Ngorongoro na kuagiza kurejeshwa huduma za kijamii, kuruhusu kufanyika kwa uchaguzi wa serikali za mitaa na kuondolewa vikwazo vyote vilivyowekwa kwa wakazi wa Tarafa ya Ngorongoro, ambao kwa siku tano wamekusanyika maeneo tofauti wakidai kupatiwa haki hizo.

kwa hisani AP

Miongoni mwa madai ya jamii ya wamaasai hao ambao awali waliandamana ni kupinga kufutwa vitongoji 96, vijiji 25 na kata 11, amri ambayo kimsingi ilikuwa ikiwakosesha haki ya kupiga kura ambayo imeratibiwa kufanyika mwezi Novemba tarehe 27, 2024

Mambo mengine wanaodai watu hao wa ngorongor kuhusu huduma za elimu, afya, barabara na maji, pamoja na kuondolewa vikwazo vya kuingia na kutoka eneo hilo

Agizo hilo la Rias Samia imetolewa iliwasilishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), William Lukuvi ambaye alizuru eneo la Oloirobi mapema leo asubuhi.

Lukuvi aliambatana na Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Danstan Kitandula, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, na Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Awadh Juma Haji

Amesema wametumwa na Rais Samia kuzungumza nao na kutoa maagizo hayo ambayo ameelekeza mamlaka zote kuanzia mkuu wa mkoa hadi wilaya kuhakikisha yanatekelezwa

wamaasai wapiga kambi eneo la Oloirobi

Aidha , Lukuvi amesema Rais amepanga kukutana na wawakilishi wa wananchi hao na kuwa utaratibu wa kukutana nao utaandaliwa ili wakawasilishe kero zao mbele yake

‘’Mkurugenzi wa Ngorongoro hawa wananchi wanapata huduma kwenye mamlaka hii lakini ziko baadhi ya huduma hazitolewi vizuri… baadhi ya shule vyoo vyake vimeharibika lakini ninyi hamshughulikii, kuna baadhi ya shule maji hayatoki, kuna shule zimeharibika lakini hamtengenezi,” Alisema Lukuvi

Aliongeza kusema “Huduma za wanafunzi zitolewe kikamilifu, huduma hospitalini lazima zitolewe kikamilifu. Nataka Makonda uhakikishe kule kote ambako huduma zimesitishwa zirejeshwe ili wananchi hawa wasipate shida kupata huduma za kijamii,” amesema