Yafichuliwa: Kampuni ya Kifahari ya Uarabuni (UAE) Yahusishwa na Uwindaji Haramu Tanzania

Mambo Muhimu Ya Kuzingatia:

  • Watoa taarifa waliozungumza na Mongabay wameeleza matukio ya uwindaji haramu kwa miongo kadhaa yanayohusishwa na kampuni ya uwindaji ya kifahari inayowahudumia watu wa kipato cha juu na familia za kifalme za Kiarabu (UAE).
  • Watu hawa wanafanya kazi katika kampuni ya Ortello au Otterlo Business Corporation (OBC), kampuni yenye makao yake Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) inaendesha uwindaji katika eneo la Loliondo, kaskazini mwa Tanzania
  • Mamlaka za Tanzania zimewasilisha notisi kadhaa za kuondolewa kwa wafugaji wa Kimaasai katika eneo la Loliondo na viunga vyake, kama sehemu ya juhudi za kupanua uwindaji na utalii wa safari.
ARUSHA, TANZANIA – MAY 19: Giraffes are seen at Arusha National Park, located between Africa’s highest mountain Kilimanjaro and Tanzania’s second highest peak Mount Meru, in Arusha region, Tanzania on May 19, 2024. The national park, hosting more than 400 animal species, offers unique nature and wildlife to its visitors. Abdulrahman Abel / Anadolu (Photo by Abdulrahman Abel / ANADOLU / Anadolu via AFP)

LOLIONDO, Tanzania

Watoa taarifa wakizungumza na Mongabay wameripoti visa vya ujangili kwa miongo kadhaa nchini Tanzania vinavyohusishwa na kampuni ya uwindaji wa kifahari inayohudumia matajiri na familia ya kifalme wa Umoja wa Falme za Kiarabu.

Watoa taarifa hawa ni kutoka kampuni ya Ortello – wakati mwingine huandikwa Otterlo – Business Corporation (OBC), ambayo inaendesha shughuli zake huko Loliondo, wilaya ya Ngorongoro kaskazini mwa Tanzania. Mahojiano na vyanzo, ambao waliomba tutumie majina bandia kutokana na kuhofia usalama wao, wametoa ufahamu wa kipekee kuhusu safari za uwindaji zilizopangwa na OBC, ambazo zilivutia wanafamilia wa kifalme wa UAE na washirika wao angalau mara moja au mbili kwa mwaka tokea miaka ya tisini hadi mwishoni mwa mwaka 2016. Wanaripoti kuwa baadhi ya safari hizi ziliishia kwa wanyama hai kusafirishwa nje ya nchi.

Usafirishaji wa wanyamapori hai umepigwa marufuku nchini Tanzania tangu mwaka 2016 ili kulinda wanyama na ndege adimu. Mnamo mwaka 2022, wabunge walibadilisha haraka uamuzi wa utata wa kuondoa marufuku hiyo ambayo ilikuwa imewekwa kwa miaka sita. Ushuhuda wa vyanzo hivyo unakuja wakati mamlaka nchini Tanzania imetoa taarifa za kuwaondoa wafugaji wa Kimaasai ndani na nje ya tarafa ya Loliondo, kama sehemu ya juhudi za kukodisha kilomita za mraba 1,500 (maili za mraba 580) za ardhi ya wamaasai kwa OBC.

Mwaka 2023, ripoti ya shirika la kutetea haki za binadamu, Amnesty International, ililaani vikosi vya serikali kwa vurugu na ukamataji wa watu wengi ambao uliwaacha takriban Wamasai 70,000 kunyang’anywa maeneo yao ya jadi ya malisho.

Ili kuthibitisha madai ya wafichuaji kwa ukamilifu iwezekanavyo, tuliona eneo la uwindaji la OBC, tukawahoji wanakijiji wa karibu na kupata nyaraka za mahakama, faili za kampuni na rekodi za usafirishaji.

Kwa mujibu wa masijala huko Dubai, OBC ilisajiliwa kama kampuni ya kigeni nchini Tanzania mwaka 1992 chini ya jina la biashara la Royal Safaris Conservation Co. LLC. Pia imesajiliwa katika mamlaka zinazofanya usajili wa kificho huko Panama na Visiwa vya Virgin vya Uingereza.

Kampuni hiyo awali ilituhumiwa kwa rushwa nchini Tanzania, na kusababisha kesi mahakamani iliyomalizika kwa makubaliano ya kukiri kosa (plea bargain). Pia imehusishwa na kufukuzwa kwa nguvu kwa Wamasai wa eneo hilo. OBC, wakurugenzi wake na mamlaka ya Tanzania hawakujibu maswali yetu tulitaka kupata maelezo yao kuhusu taarifa hizi.

Maficho ya wawindaji

Mongabay iliona eneo la uwindaji la OBC katika Pori la Akiba la Pololeti, Loliondo, na kurekodi maeneo matatu ambayo wafichuaji waliripoti yalitumiwa na wageni maalum yaani VIPs kutoka falme za Uarabuni.

Majengo haya yanaonekana vizuri katika maeneo makubwa ya pori ambapo paa, pundamilia na wanyama wengine wa pori huzurura.

Watalii wanaweza kumiminika kwenye mandhari hii kila mwaka kushuhudia makundi makubwa ya nyumbu wakihama kutoka eneo moja hali lingine. Lakini OBC inahakikisha pia kuwa mahitaji ya wale wanaopendelea bunduki za risasi kuliko kupiga picha yanatimizwa.

Eneo la OBC limegawanyika katika maeneo matatu: Chali One, eneo iliyopo kilimami na inayotumikia kama eneo kuu la matajiri iliyokamilika na  na mnara wa mawasiliano na na ulinzi madhubuti; Lima One, kituo cha kuhifadhi magari; na uwanja wa ndege wa Lima mbili pamoja na majengo.

‘Wageni’

Khalifa (jina bandia), alijiunga na OBC katika miaka ya 1990 na alifanya kazi huko kwa zaidi ya miaka 15. Mfanyakazi huyo wa zamani aliiambia Mongabay kwamba watalii wa Falme za Kiarabu walijulikana kama “wageni.”

Wote yeye na Abdulrazak (jina bandia), mfanyakazi wa sasa ambaye amefanya kazi katika OBC kwa zaidi ya mwongo mmoja, waliripoti kuwa wameshuhudia watalii wakivunja sheria za uwindaji kwenye safari zilizoandaliwa na kampuni hiyo, na kuua twiga na wanyama wengine bila kujali wakati wa ziara zao huko Loliondo.  Safari hizi zimepungua sana baada ya mwaka 2016.

“Kuna baadhi ya wanyama ambao hawaruhusiwi kuwindwa; kwa mfano, twiga hawaruhusiwi kuwindwa, kama sheria inavyosema, lakini wanawawinda. Labda hawaogopi sheria za Tanzania. Wanakuwa kama watoto; mara tu wanapoona mnyama akipita, wanachukua gari,” Abdulrazak alisema juu ya wawindaji wa utalii, akiiga sauti ya risasi na kuongeza, “Baada ya hapo, wanapiga picha.”

Alipoulizwa kwa nini hakutoa taarifa kwa mamlaka za Tanzania, Abdulrazak alisema hakufahamu kikamilifu kilichokuwa kikifanyika mwanzoni.

“Ilionekana kama wamekuwa wakifanya hivi kwa miaka mingi, lakini hatukuelewa wanachofanya,” alisema.

Abdulrazak na Khalifa walidai kwamba, walipogundua ukali wa kile kinachoendelea, waliogopa kuzungumza kwani waliamini kinaweza kuhatarisha maisha yao.

“Watu walikuwa na hofu,” Abdulrazak alisema. “Mbali na hayo, tutatoa taarifa wapi?”

Abdulrazak aliiambia Mongabay kuwa anaamini kwamba serikali ya Tanzania na polisi walikuwa wanafahamu ukiukwaji wa uwindaji wa silaha moto zilizopangwa na OBC.

Mongabay aliitaka OBC na mamlaka za Tanzania kutoa maoni juu ya madai hayo, na kueleza kama kuna ruhusa maalum zilizotolewa kwa silaha hizo za moto kutumika. Hawakuwa na jibu.

ARUSHA, TANZANIA – MAY 19: A bird perches on a giraffe at Arusha National Park, located between Africa’s highest mountain Kilimanjaro and Tanzania’s second highest peak Mount Meru, in Arusha region, Tanzania on May 19, 2024. The national park, hosting more than 400 animal species, offers unique nature and wildlife to its visitors. Abdulrahman Abel / Anadolu (Photo by Abdulrahman Abel / ANADOLU / Anadolu via AFP)

Kwa ukatili mkubwa bila kujali

Akiwa Chali One, eneo la kilima, Abdulrazak alisema alishuhudia mwanafamilia wa kifalme wa Dubai akimpiga risasi twiga ambaye alitangatanga karibu sana na nyumba ya kuwinda.

“Niliiona kwa macho yangu mwenyewe,” aliiambia Mongabay.

Twiga wa Masai (Giraffa tippelskirchi), ni mnyama maalum kwani nembo ya taifa ya Tanzania na ameorodheshwa kuwa hatarini kupotea katika orodha ya shirika la kuhifadhi ya Wanyama ya IUCN. Wahifadhi wanalaumu uwindaji haramu, magonjwa na uvamizi wa ardhi kwa idadi ya twiga hao kupungua.

Adhabu ya kumuua twiga katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki ni pamoja na faini ya hadi dola 15,000 na kifungo cha miaka kadhaa jela.

Hata hivyo kwa mujibu wa Abdulrazak, hakuna hatua zozote za utekelezaji zilizochukuliwa. Badala yake, alisema kuwa nyama kutoka kwa mnyama aliyeuwawa ilitumwa Dubai.

Abdulrazak aliongeza kuwa alimuona mgeni huyo, ambaye alimwelezea kuwa anajulikana miongoni mwa wafanyakazi wa kambi hiyo, mapema siku hiyo.

“Hakujitambulisha lakini tulimjua kwa jina lake,” alisema, akisisitiza kwamba anaweza kumtambua mtu huyo katika umati wa watu 500.

Mongabay ilimuomba mfanyakazi huyo wa OBC kumtambua mtu huyo kutoka kwenye rundo la picha, na alifanya hivyo.

Abdulrazak aliendelea kuongeza kuwa matukio kama hayo ni ya kawaida miongoni mwa wawindaji maalum wa VIP, ambao, kama wenyeji, hutumia bunduki, mitego na mbwa kuwinda twiga kinyume na kanuni za wanyamapori zinazolinda wanyamapori.

Mizigo ya wanyama

OBC ilianzishwa na Jenerali Mohammed Abdulrahim Al Ali, Emirati. Picha za BRELA, Msajili wa makampuni Tanzania, zinaonyesha kuwa anahudumu kama mkurugenzi wa Royal Safaris Conservation Co. LLC., jina la biashara la OBC, pamoja na raia wa nchi hiyo Khamis Mohamed Sultan bin Shaheen Al Suwaidi. Watu hao wawili hawakujibu maombi yetu ya kutoa maoni.

Kwa mujibu wa Abdulrazak, Al Ali alikuwa dalali mkuu wa safari za uwindaji za matajiri kutoka Falme za Kiarabu (UAE) nchini Tanzania hadi mwaka 2016; Hasa, alikuwa na jukumu la kupanga kukamata na kusafirisha wanyama hai, hasa simba na chui. Haijulikani ni mara ngapi, kwa maana vitendo hivi vilikuwa vya mara kwa mara, au bado vinaendelea.

Katika kipindi hiki, Al Ali alifanya kazi kwa karibu na Abdulrahman Kinana, makamu mwenyekiti wa zamani wa chama tawala cha Tanzania cha Chama Cha Mapinduzi (CCM), wandani wa OBC walieleza. Waliongeza kuwa Kinana alifanya kazi kama mwakilishi wa serikali ya Tanzania wakati wa ziara kutoka kwa matajari wa Falme za Kiarabu.

Kwa mujibu wa wandani wa kampuni hiyo, Kinana na Al Ali waliratibu maandalizi ya kuwasili kwa wageni hao, na kuwaagiza walinzi kutambua maeneo ya wanyama wanaovutia. Wahusika wote wawili hawakujibu ombi la kutoa maoni.

“Abdulrahman Kinana daima yupo, hata wakati Al Ali anapotembelea kabla ya wageni [kuwasili],” Abdulrazak alisema.

Mara kadhaa, safari hizi za uwindaji ziliishia kwa watalii kumuua mnyama wa kike na kumkamata mtoto wake na kumtunza katika kituo cha kuhifadhi cha Lima One, kulingana na vyanzo.

“Kama watakuona barabarani, wanakusimamisha na kuuliza ni wapi umeona chui, simba au mbuni,” Abdulrazak alisema kuhusu watalii hao. “Wanapenda sana wanyama wachanga kwa sababu wanyama wakubwa ni vigumu kusafirisha.”

Wakizungumza kwa masharti ya kutotajwa jina, wakazi wa Kirtalo na Ololosokwan, vijiji viwili karibu na Pori la Akiba la Pololeti, waliiambia Mongabay kuwa wameshuhudia wafanyakazi wa OBC wakisafirisha wanyama hai kupitia ndege mwaka 2022 na 2023. Abdulrazak alisema kuwa OBC ilisafirisha wanyama hai kutoka Loliondo.

Kwa mujibu wa vyanzo viwili ndani ya OBC, wanyama wamekuwa wakisafirishwa mara kadhaa kutoka hifadhi hiyo hadi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kwa ndege nyepesi yenye uwezo wa kubeba vizimba kadhaa vya wanyama. Katika uwanja wa ndege, Al Ali na Kinana walisimamia upakuaji wa vizimba hivi ambavyo vilipakiwa kwenye ndege ya mizigo kuelekea Dubai, walisema.

“Wakati wageni wanaondoka, ndege ya mizigo inaendelea kuchukua wanyama. Al Ali anaondoka na ndege ya mwisho baada ya ndege ya mizigo kuondoka,” Abdulrazak alisema.

Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), ambayo ilisimamia uwanja huo mwaka 2023, haikujibu ombi la Mongabay la kutaka kupata maoni yao.

Kukimbia au kupambana

Kesi katika Mahakama Kuu ya Tanzania mwaka 2018 inatoa mwanga zaidi juu ya shughuli za OBC.

Kampuni hiyo iliingia katika mgogoro na watu saba ambao walidai kulipwa na kampuni hiyo kusafirisha wanyamapori kupitia uwanja wa ndege. Kwa mujibu wa nyaraka zilizowasilishwa mahakamani, ambazo hazikutaja wazi mzigo ulioshughulikiwa, watu hawa saba ilisema kuwa ajira yao ya OBC ilisitishwa kwa haki mnamo 2016 na kudai fidia na stahiki zao. Kampuni ya Viwanja vya Ndege vya Kilimanjaro (KADCO), ambayo hadi hivi karibuni iliendesha KIA, ilikuwa imewapa pasi za usalama, nyaraka zinaonyesha.

Mahakama iliwapa hukumu ya kupewa malipo na stahiki wafanyakazi hawa, lakini uamuzi wa baadaye uliotolewa uliangukia upande wa OBC baada ya kampuni hiyo kudai haikuajiri walalamikaji hao saba. Kama ushahidi, ilitoa orodha ya wafanyakazi ambao ilisema waliajiriwa katika kipindi cha mwaka 1998 hadi 2016.

Swali la nani alikuwa amependekeza KADCO iwape pasi za usalama – OBC au kampuni inayoshughulikia mizigo katika uwanja wa ndege – haikujibiwa

Uhusiano wa karibu bado

Ingawa ziara za kifalme zimeripotiwa kupungua tangu mwaka 2016, OBC bado ina uhusiano wa karibu na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Rekodi rasmi za mauzo ya nje ya Tanzania zilizopatikana kutoka kwenye kanzidata ya biashara ya kimataifa zinaonyesha kuwa mwaka 2023, OBC ilisafirisha shehena 72 za nyama ya wanyama pori, au bushmeat, kutoka Tanzania kwa angalau wakazi wa Falme za Kiarabu nne, ikiwa ni pamoja na viongozi wa biashara na washirika wanaojulikana kuwa karibu na familia za kifalme wa UAE.

Tanzania ilihalalisha mauzo ya nyama pori chini ya sheria kali mwaka 2020. Mongabay iliwasiliana na wapokeaji wa usafirishaji huo na kuuliza maswali kuhusu mauzo ya nje, ikiwa ni pamoja na vibali muhimu walivyokuwa navyo.

Hakuna hata mmoja wa wapokeaji wanne aliyejibu maswali yoyote ya Mongabay, na mmoja alitaja usiri kama sababu ya kukataa kutoa maoni. Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania pia haikujibu maswali ya Mongabay kuhusu uhalali wa mauzo ya nje. Pia OBC haikujibu.

Shida ya zamani

Shughuli za uwindaji wa matajiri kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) zilianza mwaka 1992, wakati serikali ya Tanzania ilipokodisha eneo la ardhi lenye ukubwa wa kilomita 4,000 (1,544-mi2) huko Loliondo kwa raia wa UAE aliyetambuliwa kama Brig. Gen. Mohammed Abdulrahim Al Ali.

Ardhi hiyo ambayo ina eneo la km mraba 1,500 ambalo mamlaka sasa inataka kukodisha, iliunda kile kilichoitwa Pori tengefu la Loliondo. Ikawa eneo la madhumuni mengi kwa ajili ya uwindaji, uhifadhi na ufugaji.

Masharti ya mkataba huo yalikuwa siri ya serikali iliyolindwa kwa ukaribu. Lakini baadaye iliibuka katika ripoti ya tume ya serikali kuhusu ufisadi kwamba afisa aliyewaidhinisha alifanya hivyo kufuatia shinikizo kutoka kwa viongozi wa juu “kwa msingi kwamba yeye [Al Ali] alikuwa rafiki.”

Kufuatia ukosoaji katika vyombo vya habari kuhusu makubaliano haya ya siri, hasa kupitia makala za mwandishi wa habari wa gazeti la Mfanyakazi Stan Katabalo, zilichochea kashfa hii  kujulikana kama “Loliondogate,” Al Ali alianzisha OBC kama njia ya kurasimisha mpango huo.

Kufikia mwaka 1994, Abubakar Mgumia, waziri wa utalii wakati huo, alikabiliwa na shinikizo wakati taarifa za mkataba huo wa siri zilipovuja. Kutokana na hali hiyo, serikali ilianzisha Tume ya Marmo mwaka huo kuchunguza mkataba huo ulioko Loliondo. Mgumia alifukuzwa kazi, lakini shughuli za OBC zilionekana kuwa haziathiriwi.

Miaka miwili baadaye, Rais Benjamin William Mkapa aliunda Tume ya Warioba, kufanya uchunguzi mpana kuhusu ufisadi huu. Pia, iligundua kuwa leseni ya OBC ilikuwa kinyume cha sheria na iliunga mkono matokeo ya Tume ya Marmo kwamba rushwa ilihusika katika ugawaji wake.

Leseni ya uwindaji ya OBC ilifutwa mwishoni mwa mwaka 2017 kutokana na madai zaidi ya rushwa na ufisadi. Waziri wa Maliasili na Utalii wa wakati huo, Hamis Kigwangalla, alimshutumu Isack Mollel aliyekuwa mkurugenzi mtendaji wa OBC, kwa kujaribu kuihonga wizara yake kwa michango yenye thamani ya zaidi ya dola za kimarekani milioni mbili (2).

Mollel alikamatwa mara moja na kufunguliwa mashtaka ya uhujumu uchumi. Kulingana na makala iliyochapishwa mnamo Aprili 2024 kwenye gazeti la The Atlantic, kesi hiyo ilimalizika kwa makubaliano maalum ya kukiri kosa (plea bargain).

Unyang’anyi wa ardhi

Wanaobeba mzigo ya wawindaji wa kitalii katika eneo la Loliondo ni wafugaji wa Kimaasai ambao wamekuwa wakifurushwa mara kwa mara kutoka katika mashamba yao ya asili ya malisho tangu mwaka 1959, walipohamishwa huko kutoka Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Wengi wa wale waliohamishwa sasa wanaishi katika maboma ya kiasili ambayo huvutia watalii wa kigeni kwa fursa za picha.

Mamlaka za kikoloni ziliwalazimisha Wamaasai kutoka katika maeneo yao ya jadi katika hifadhi ya taifa ya Serengeti na kujiunga na Hifadhi ya Taifa ya Tarangire ili kuhifadhi maeneo hayo kwa ajili ya uwindaji maalum. Wamaasai wameishi katika vijiji vilivyo kwenye viunga vya mbuga.

Hata hivyo uhakika wa kuishi hapo haukuwa wa kudumu. Vikosi vya usalama viliwafurusha wanajamii katika vijiji vinne ambavyo ni Arash, Kirtalo, Oloirien na Ololosokwan na kupeleka vikosi kuwahamisha kwa nguvu mwaka 2009, 2013 na 2017, kwa mujibu wa shirika la haki za binadamu la Amnesty International.

Msako huo uliendelea baada ya agizo la rais mwaka 2022 kutangaza kuwa eneo la Pori tengefu la Loliondo (Game Controlled Area) litakuwa Pori la Akiba (Pololeti), na kuviondoa vijiji 14 katika mchakato huo.

Mwaka huo, katika eneo la Ololosokwan, wilayani Ngorongoro, makabiliano makali yalishuhudiwa wakati polisi walifyatua risasi dhidi ya umati wa waandamanaji, na kuwajeruhi Wamaasai kadhaa. Afisa wa polisi pia aliuawa kwa kutumia mshale.

Siku chache baadaye, mamlaka nchini Tanzania ilitangaza kuwa eneo la hifadhi ya Ngorongoro litageuzwa kuwa hifadhi ya wanyama ambapo wafugaji hawataruhusiwi kuishi.

Aidha, Januari mwaka huu, serikali ya Tanzania iliongeza kampeni yake ya ukatili katili dhidi ya wafugaji wanaoishi karibu na maeneo yaliyohifadhiwa katika Bonde la Ufa. Askari wa wanyamapori walifyatua risasi kwa wafugaji wa Kimaasai na kukamata ng’ombe katika wilaya ya Simanjiro, karibu na Hifadhi ya Taifa ya Tarangire.

Mongabay awali iliripoti kuwa, mnamo Machi 2024, mamlaka za Tanzania zilitoa matangazo mapya ya kufuta makazi yaliyoathiri jamii za Wamaasai. Wimbi la kwanza, kwa upanuzi wa Hifadhi ya Taifa ya Tarangire, lililenga wilaya ya Simanjiro. Ya pili iliathiri vijiji nane kupanua uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (KIA).

 

This article is reproduced in Kiswahili with permission from Mongabay.