Zaidi ya wasichana na wanawake milioni 79 waishio kusini mwa Sahara wamekumbana na ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia wakiwa watoto.
Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia watoto limesema takwimu mpya zilizokusanywa zinaonyesha kuwa eneo hili ni miongoni mwa sehemu mbaya zaidi duniani kwa wasichana.
Duniani kote, UNICEF inakadiria kwamba unyanyasaji wa kijinsia umewakumba wasichana na wanawake wapatao milioni 370, huku takriban mmoja kati ya watano aliyopo Kusini mwa Sahara akipitia unyanyasaji wa kijinsia au ubakaji kabla ya kufikisha umri wa miaka 18.
“Unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya watoto ni aibu kwa tamaduni zetu ,” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF, Catherine Russell.
Kutoa takwimu kama hizi ni mara ya kwanza, zikiwa zimehesabiwa kwa kutumia data za kitaifa na programu za utafiti wa kimataifa kutoka mwaka 2010 hadi 2022, alisema Claudia Cappa, mtaalamu mkuu wa takwimu wa UNICEF.
Alisema kuna mapungufu katika data hiyo, pamoja na ukosefu wa ripoti kutoka baadhi ya nchi.
“Ni ya kutisha,” alisema Nankali Maksud, mtaalamu wa unyanyasaji wa watoto katika eneo la Nairobi. “Ni vizazi vya maumivu.”
Matokeo ya maumivu haya yana madhara makubwa kwa maendeleo.
“Tunatoa nguvu nyingi kuhamasisha wasichana kuingia shuleni, lakini msichana aliyebakwa au aliyepitia unyanyasaji wa kijinsia hawezi kujifunza,” alisema Maksud.
Takwimu hizo ni za juu zaidi katika maeneo yaliyoathirika na migogoro na kutokuwa na usalama. Mashirika ya misaada nchini Sudan yameonya kuhusu hatari kwa wasichana na wanawake kutokana na migogoro inayoendelea huko.
“Watoto katika mazingira dhaifu wako katika hatari kubwa zaidi ya unyanyasaji wa kijinsia,” alisema Russell. “Tunashuhudia unyanyasaji wa kutisha wa kijinsia katika maeneo ya mizozo, ambapo ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia mara nyingi vinatumika kama silaha za vita.”
Wajibu wa kwanza walieleza kwa Shirika la Human Rights Watch mapema mwaka huu kwamba idadi ya kesi zilizoripotiwa ni sehemu tu ya idadi halisi, huku wengi wa waathirika wakiwa hawawezi au hawataki kutafuta huduma za dharura.