Chama cha upinzani Tanzania Chadema kimeitisha kikao cha dharura kesho, Ijumaa, Novemba 29, 2024 kujadili uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji, uliofanyika nchini kote jana, Novemba 27, 2024
Taarifa kwa umma iliyotolewa leo Alhamisi, Novemba 28, 2024 na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema, imesema kikao hicho kitaongozwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe
Mrema amesema kikao hicho kitajadili agenda maalumu yaliyojiri kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji uliofanyika jana Jumatano, Novemba 27, 2024.
Katika uchaguzi huo, baadhi ya mambo ambayo Chadema imekilalamikia ni matukio ya mauaji ya wagombea wake. Wagombea hao ni mgombea ujumbe Mtaa wa Ulongoni A jijini Dar es Salaam, Modestus Timbisimilwa anayedaiwa kuuawa kwa kupigwa risasi na Polisi
Mwingine ni aliyekuwa mgombea uenyekiti wa Kitongoji cha Stand katika Jimbo la Manyoni Mashariki mkoani Singida, George Mohamedi anayedaiwa kuuawa kwa kupigwa risasi
Mambo mengine ambayo chadema imelalamikia katika uchaguzi wa jumatono ni uwepo wa makaratasi feki ya kupigia kura, hujuma, mawakala wa upinzani kuondolewa katika vituo vya kupigia kura, wizi, wasimamizi wa uchaguzi kukimbia na masanduku ya kupiga kura, majina yawapiga kura na wagombea kukosekana na vile vile wagombea kuengulia kwa kutumia sifa sisizofa.
Mkutano huo utafanyika katika makau makuu ya chama hicho mikocheni, Dar es salaam ambapo chama itatoa kauli rasmi.