Ni Mbowe, Lissu au Odero kuongoza Chadema?

Waswahili wanasema leo ndio leo, inyeshe mvua liwake jua lazima kieleweke hivi ndivyo unaweza kusema leo katika Mkutano Mkuu wa Chadema ambapo wanachadema wanaamua hatma yao katika safu yao ya uongozi ni nani ataongoza gurudumu la chadema kama Mwenyekiti Taifa.

Mchuano wa nafasi ya Mwenyekiti Taifa ni kati ya Freeman Mbowe, Tundu Lissu na Odero Charles Odero, ingawa  mchuano umekuwa mkali zaidi kati ya Lissu na Mbowe hapa ni hiari ya wajumbe katika maamuzi yao

Wawili hawa wabobevu katika siasa nchini Tanzania wanasaka nafasi ya uenyekiti kila mmoja akiwa na sera zake ambapo upande wa Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema kwa zaidi ya miaka 20 anadai kuwa bado anakazi hajamaliza na kwamba anatamani kukijenga chama zaidi licha ya umri wake kumtupa mkono sasa. 

Mjadala mzito uliibuka na kuibua hisia mseto kwa wafatiliaji wa siasa ndani na nje ya nchi lakini hofu kubwa ni juu ya ustawi wa chama hicho kilichojegwa kwa miongo mitatu sasa.

Kwa sasa kuna makundi ndani ya chama hicho ambapo wapo wanaomuunga mkono Lissu na wapo wanaomuunga mkono Mbowe, sasa swali ni je makundi hayo yatakuja pamoja baada ya uchaguzi au ndio kusambaratika kwa chama kunaanzia hapo.

Lakini yote kwa yote kila mmoja ana matumaini ya ushindi kutokana na anavyoona.

Je ni Odero? Mbowe? au Lissu majibu wanayo wajummbe wa mkutano huo.