Miaka 48 ya CCM, yaendelea kushika dola

Chama tawala nchini Tanzania Chama cha Mapinduzi(CCM) leo kinaadhimisha miaka 48 ya kuzaliwa kwake huku kikijivunia kuendelea kushikilia dola nchini humo.

Leo hii chama hicho kimekuwa na sherehe kubwa jijini Dodoma ambapo wana CCM wakiongozwa na viongozi wakuu wa chama hicho akiwemo Mwenyekiti wa chama Taifa Samia Suluhu Hassan.

Katika Sherehe hizo pamoja na mambo mengine yaliyopangwa kufanywa CCM, itawatambulisha rasmi wagombea wao wa Urais 2025 ambaye ni Rais Samia Suluhu na mgombea mwenza Emmanuel Nchimbi ambaye ni Katibu Mkuu.

Kadhalika itamtambulisha Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Mwinyi kama mgombea Urais kwa upande wa visiwani Zanzibar.

Wote hao walipitishwa na vikao vya juu vya CCM vilivyofanyika Januari 18 na 19,2025 kuwa wagombea Urais.