Kesi ya kusambaza taarifa za uongo kwenye mtandao wa X zamani Twitter inayomkabili Dk Willibrod Slaa(76) itatajwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam.
Dk Slaa ambaye ni mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania anadaiwa kutenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 16 cha sheria ya Makosa ya Mtandao namba 14 ya mwaka 2015.
Hii leo inatajwa kwa ajili ya kuangaliwa iwapo upelelezi wa kesi umekamilika, ingawa imefungwa mikono kuendelea na hatua zaidi baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini kuwasilisha kusudio la kukata rufaa katika Mahakama ya Rufani kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu kuhusu kupatikana kwa dhamana ya mshtakiwa kutokana na kuangalia uhalali wa kesi ya jinai kwa haraka.
Hivyo kwa mujibu wa sheria kesi hiyo kwa kuwa mshtakiwa yupo rumande kutokana na upande wa mashtaka kuweka zuio la dhamana kesi hiyo itakuwa inatajwa kila baada ya siku 14 hadi pale itakapopatiwa ufumbuzi katika Mahakama ya Rufani.
Dk Slaa alipandishwa Kisutu kwa mara ya kwanza Januari 10, 2025 na kusomewa shtaka moja la kusambaza taarifa za uongo katika Mtandao wa X.
Inadaiwa kupitia mtandao wa X kwa jina la Maria Sarungi Tsehai @MariaSTsehai , Dk Slaa aliandika ujumbe uliosomeka”Wakubwa wametafutana, nikisema wakubwa namaanisha Mwamba na Samia, na wala hatuna maneno ya kumung’unya na kimsingi wamekubaliana Suluhu Samia amekubali atatoa pesa, Suluhu Samia ataongeza nguvu ya pesa, ni dhahili atatoa pesa, hizo hela ni za Watanzania wanazichezea Samia na watu wake”
Lakia pia kupitia jukwaa hilo pia aliandika ”Samia toka muda mrefu haangaikii tena maendeleo ya nchi, anahangaikia namna ya kurudi Ikulu, na namna yake ya kurudi Ikulu ni kwa njia hizo kama kumsaidia mtu kama Mbowe”
Dk Slaa anatetewa na Wakili Boniface Mwabukusi, Wakili Hekima Mwasipu, Edson Kilatu, Peter Madeleka, Sanga Melikiole, Sisty Aloyce na Mwanaisha Mndeme.
Jopo la mawakili wa serikali linaongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi Tawabu Issa, Clemence Kato, Michael Ngoboko, Nura Manja wakisaidiana na mawakili wa Serikali Abdon Bundala na John