Golugwa: Uchaguzi wa 2024 Ulikuwa Chanzo cha Msimamo wa “No Reforms, No Elections”

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, Amani Golugwa, ameanza kutoa ushahidi katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu, akieleza kuhusu nafasi yake ndani ya chama na matukio ya uchaguzi yaliyotangulia msimamo wa “No Reforms, No Elections”.

 

 

Golugwa, mwenye umri wa miaka 47, amesema amekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Bara tangu Januari 22, 2023, baada ya kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi ndani ya chama hicho. Amesema kabla ya nafasi hiyo alikuwa Katibu wa Kanda ya Kaskazini, akisimamia mikoa ya Tanga, Arusha, Kilimanjaro na Manyara.

Huyu ni shahidi wa tatu wa upande wa utetezi dhidi ya Lissu, ambaye ameanza leo kutoa ushahidi wake.

Katika ushahidi wake, Golugwa ameeleza pia kuwa mwaka 2020 aliteuliwa kuwa meneja wa kampeni wa aliyekuwa mgombea urais wa CHADEMA, Tundu Lissu, huku akisema amekuwa mwanachama wa chama hicho tangu mwaka 2007. Ameeleza pia kuwa ana elimu ya Diploma ya Uhasibu kutoka Chuo cha Uhasibu Arusha na aliwahi kufanya kazi za uhasibu kati ya mwaka 2011 na 2015.

Akizungumzia mkutano wa Aprili 3, 2025 ambao Jamhuri inadai Lissu alitoa kauli zenye nia ya kuitishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Golugwa amesema anaifahamu mikutano hiyo na kwamba iliandaliwa na Sekretarieti ya chama.

Amesema lengo lilikuwa kuwaeleza watia nia msimamo wa chama wa “No Reforms, No Elections”, uliotokana na malalamiko kuhusu mwenendo wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2024.

Hapa ni sehemu ya maswali na majibu kati ya Shahidi na Mshtakiwa

Lissu:Umekuwa kwenye nafasi hiyo toka lini?Golugwa:Kabla ya kuwa kwenye nafasi hii nimekuwa Katibu wa Kanda ya Kaskazini toka mwaka 2013 February mpaka nilipothinitishwa kuwa Naibu Katibu Mkuu

Lissu:Unaposema Katibu wa Kanda ya Kaskazini unamaanisha niniGolugwa:Namaanisha mikoa minne, mkoa wa Tanga, Arusha, Kilimanjaro na Manyara hiyo ndio maana ya Kanda ya Kaskazini

Lissu:Waeleze Waheshimiwa majaji kabla ya kuwa Katibu wa Kanda ya Kaskazini ulikua na nafasi gani Golugwa:Nimeshika pia nafasi ya Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha. Na pengine nitumie maneno vizuri kwamba kutoka 2014 mpaka2019 nilikuwa Mwenyekiti mkoa wa Arusha. Na kabla ya hapo kutoka 2008 mpaka 2014 nilikua Katibu wa Mkoa wa Arusha

Lissu:Waeleze Waheshimiwa majaji kama kuna nafasi nyingine ya kichama uliwahi kushikilia Golugwa:Waheshimiwa majaji mwaka 2020 niliteuliwa na chama kuwa Kampeni meneja wa Aliyekuwa mgombea Urais Mh. Tundu Lissu.

Lissu:Sasa umekuwa ndani ya hiki chama kwa miaka mingapi?Golugwa:Nimeingia kwenye chama hiki toka 2007 mpaka leo nimekuwa mwanachama wa chama hiki.

Lissu:Naomba uwaeleze Waheshimiwa majaji mtu anapataje nafasi ya Naibu Katibu wa Chadema a BaraGolugwa:Ili mtu kuwa Naibu Ktibu Mkuu wa Chadema mbali na uanchama wake kuaminika jina lke litapendekezwa na Mwenyekiti, maana yake mwenyekiti atapendekeza mtu ambaye anaona ana uwezo na jina lake litapelekwa mbele ya Baraza la Chama, na kisha wajumbe wa Baraza Kuu watafanya wajibu wao wa kuthibitisha wasifu na uwezo huyo Mwanachama aliyependekezwa

Lissu:Waeleze Waheshimiwa majaji majukumu ya Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Golugwa:Wajibu wa Naibu Katibu Mkuu Chadema kwanza ni Msaidizi wa Katibu Mkuu anamsaidia Katibu Mkuu, Pili ndie mwandishi wa kumbukumbu za vikao vya chama na tatu Naibu KatibuwMkuu amepewa mwongozo kwenye itifaki ya chama kwamba ndie mkuu na msimamizi wa itifaki ya chama katika vikao na mikutano ya chama

Lissu: Sasa Shahidi tuache hayo ya wasifu ya chama kidogo, Waeleze Waheshimiwa majaji wasifu wako wa kitaaluma Golugwa:Waheshimiwa Majaji, Elimu yangu ya chuo nimesoma masula ya UhasibuLissu:Umesoma Uhasibu ktika chuo gani Golugwa:Nimesoma Katika Chuo cha Uhasibu Arusha akiwa ngazi ya Diploma

Lissu:Sasa mi naskia kuna makelele kwenye masual ya chama nataka uwaeleze Waheshimiwa majaji uzoefu wako katika kazi hiyo ya Uhasibu Golugwa:Nimefanya kazi ya Uhasibu nikianza na ngazi ya Account Assistant na nimefanya kazi ya Uhasibu toka 2011 mpaka 2015 kwenye maeneo tofauti tofauti.

Lissu:Nataka tuzungumzie kesi, hii kesi ya Uhani inayonikabili, ninayuhumiwa kwamba kwenye mikutano uliofanyika trh 3 Aprili 2025 Nilitoa maneno yenye nia ya kuitishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano yanasema hivi  “wanasema kitu kimojawsahihi hapa, wanasema hivii msimamo huu unaashiria uasi ni kweli tutahamasisha Uasi…… Swali langu Waeleze Waheshimiwa majaji kama unaufahamu huu mkutano Golugwa:Huo mkutano nina ufahamu

Lissu:Waeleze Waheshimiwa majaji huo mkutano uliandaliwa na nami nanulifanyikia wapi Golugwa:Huu mkutano uliandaliwa na Sekretalieti ya chama baada ya Katibu Mkuu kuleta wazo kwenye Sekretalieti kwamba Watia nia ni Wadau Muhimu hivyo tuandae mkutano tukutane nao na Sekretalieti ikafanya maandalizi na mkutano ukafanyika kwenye ukumbi wa makao makuu ya chama mikocheni Dar es salaam

Lissu:Unasema kwamba mkutano uliandaliwa na Sekretalieti, Waeleze Waheshimiwa majaji hii Sekretalieti ni akina nani Golugwa:Hii Sekretalieti ninayoizungumzia ni Katibu Mkuu wa Chama, Manaibu Katibu wawili kwa maana ya Bara na Zanzibar, Makatibu wa Mabaraza matatu ya chama, BAWACHA, BAVICHA na BAZECHA.Pia Wakurugenzi wa Chama pamoja na wataalam wawili ambao wameteuliwa na Mwenyekiti kuwa sehemu ya Sekretalieti ya chama

Lissu:Jumla watu wangapi hapo kwa hesbau yako  Golugwa:14Lissu:Kwa muundo wa Chama Sekretalieti ya Chadema ni chombo cha aina gani Golugwa:Sekretalieti ya Chadema ndicho chombo cha kiutendaji kinachofanya kazi kila siku za kichama kwa niaba ya Kamati Kuu ya Chama.

Lissu:Sasa Shahidi umesema Katibu Mkuu alikuja na wazo kwamba muandae mkutano muwaandae watia nia hao watia nia ni akina nani?Golugwa:Hao watia nia ni wanachama wa Chadema ambao audha walipiyoshwa kuwa wagombea kwenye uchaguzi wa 2020 katika nafasi za udiwani, ubunge na Urais na kwamba bado nia yao ya kutaka kugombea nafasi hizo bado walikuwa nayo. Na wengine katika kundi hilo la watia nia ni wale ambao hawajawahi kugombea wala kupitishwa kwenye nafsi hizo nilizozitaja kwa maana mwaka 2025 na wao wakataka kutia nia wapitishwe kugombea nafasi hizo. Hao ndio watia nia.

Lissu:Waeleze Waheshimiwa majaji hao watia nia walikua wanatia nia ya kugombea nafasi gani Golugwa:Waheshimiwa majaji hao watia nia walikuwa wanatia nia ya kugombea kwenye uchaguzi wa mwaka 2025.

Lissu:Waeleze Waheshimiwa majaji lengo la kuwaita hao watia nia kwenye huo mkutano wa trh 3 Aprili lilikuwa lengo gani?Golugwa:Lengo lilikuwa ni kuwaeleza na kuwafafanulia juu ya msimamo wa Chama uliopitishwa na Mkutano kwa maana ya wazo la No Reforms No Elections, na msimamo huo ukawa umefafanuliwa na Kamati Kuu ya chama kwa kuazimiwa hilo ndilo lilikuwa lengo.

Lissu:Waeleze Waheshimiwa majaji Unaposema No Reform No Elections, huu msimamo ulikuwa unahusu nini hasa?Golugwa:Msimamo huu ulianza au ulizaliwa baada ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Mwaka 2024.Nikiwa Katibu wa Kanda ya Kaskazini, Katibu Mkuu alituambia Makatibu wa Kanda  tuandike ripoti ya uchaguzi wa Serikali za mitaa jinsi ulivyofanyika, na mimi kama mtendaji ambaye nilikuwa sehemu ya uchaguzi huo kwa kusimamia kanda ya Kaskazini nilitoa ripoti kwa kuonyesha madudu mengi ya hivyo yaliyojitokeza. Na katibu Mkuu alitutaka tuandike maoni yetu ya kuhusiana na nini chama kifanye kutokana na hayo yaliyojitokeza, kwa hivyo mimi kwenye ripoti niliandika na Waheshimiwa majaji naomba nitumie maneno Exactly maneno niliyoandika yalikuwa maneno makali “Kwa ushenzi huu niliouona chama kisishiriki uchaguzi mwingine wowote mpaka kushinikiza mabadiliko kwenye mifumo ya uchaguzi”.

Na Makatibu wenzangu kutoka katika kanda 9 kila mmoja kwa lugha yake wote tulitoa taarifa au ripoti yenye pendekezo zinazofanana na ndipo Kamati Kuu ikaketi ikayachakta mapendekezo ya Makatibu wa Kanda na wajumbe wenyewe wa Kamati Kuu ikatafakari kwa jinsi wanavyojua, basi nadhani tarehe 10 December 2024, Mwenyekiti wa Chama wakati huo Mh. Freeman Mbowe akatoa tamko rasmi ya chama, msimamo wa Kamati Kuu yaliyoazimiwa kwamba hatutakuwa tayari kwenda kwenye uchaguzi mwingine wowote bila mabadiliko kwenye mifumo ya uchaguzi.

Lissu:Shahidi ebu Waeleze Waheshimiwa majaji kwa kifupi ni ushenzi gani uliouona Golugwa:Waheshimiwa majaji ushenzi ni mwingi.

Lissu:Suala la wateuzi wa wagombea lilikuaje Golugwa:Kwenye uteuzi wagombea Chadema na wa vyama vingine vya Upinzani kulikua na matatizo kuanzia kwenye kuchukua ile fomu ya Tume, watumishi wa Tume walikuwa wanawakwepa wagombea wetu, kwa makusudi hawawapi fomu, kwa makusudi walikuwa wanakataa kupokea fomu, na pindi tunapotaka kurudisha fomu watumishi wa tume walikua wanashirikiana na wagombea wa CCM kuzitengeneza sababu ili wasiwape fomu wagombea wetu.Utawekewa pingamizi la hujui kusoma na kuandika utaenguliwa, utawekewa pingamizi la Urais utaenguliwa.

Lissu:Waeleze Waheshimiwa majaji utaratibu wa Mawakala wa wagombea au wa Vyama ulikuaje kwenye uchaguzi huo.Golugwa:Waheshimiwa majaji utaratibu wa Mawakala ambao kimsingi wanamuwakilisha mgombea na Chama ulihitaji Wakala kwenda kuapishwa kwenye ofisi ya Kata akiwa na barua ya chama na baada ya uapisho ule, kile kiapo kinabaki pale na kwamba siku ya uchaguzi msimamizi ndiye atakayepewa kwa hiyo wakala utambulisho wake utapelekwa kwenye kituo, halafu wakala atakpokwenda kwenye kituo cha kura ndio atakuta kiapo chake.

Lissu:kilitokea nini Golugwa:Na hapo ndipo kwenye tatizo, Mawakala wa Chadema walipokwenda kwenye vituo hawakukuta hivyo viapo ambavyo ndio utambulisho wao ila utambulisho wa CCM upo mle ndani

Lissu:Matokeo yake yalikuaje Golugwa:Na hapo ndipo tatizo, Mawakala wetu wakazuiwa kuingia kwenye vituo vya kupiga kura, wakaambiwa nendeni kwa Mkurugenzi na huo muda ambao Mawakala wetu hawakuwepo ndipo huo ushenzi ukafanyika.

Lissu:Matokeo ya uchaguzi wa vijiji na mitaa mwaka 2024 yalikuaje baada ya ushenzi wote huo Golugwa:Waheshimiwa majaji kwa kumbukumbu zangu za nchi nzima CCM walishinda kwa asilimia 99.2 ya vijiji na vitongoji vya mitaa yote, Chadema na Vyama vya Upinzani waliambulia 0.8 ya asilimia zote. Na kwa kanda ya Kaskazini ambapo nilikua Katibu wa Kanda CCM walishinda kwa asilimia 98.7 kati ya vijiji, mitaa na vitongoji vya kanda ya Kaskazini

Lissu:Sasa shahidi Waeleze Waheshimiwa majaji tofauti ya uchaguzi huo wa 2024 na uchaguzi huo wa mwaka 2019 wakati wa John Pombe Magufuli.Golugwa:Waheshimiwa Majaji  hapakuwa na tofauti yoyote ya mambo yaliyotokea isipokua kuna jambo moja, 2019 hata suala la kurudisha fomu zile lilikuwa ni vita na sehemu kubwa fomu za wagombea wa Chadema zilikataliwa kwahiyo hali ilikua ni vilevileLissu:Waeleze Waheshimiwa majaji kanuni za kuendesha huo uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Vijiji zilitungwa na nani Golugwa:Kanuni za uendeshaji wa uchaguzi huo zilitungwa na Waziri wa TAMISEMI wakati huo Mohamed Mchengerwa Lissu:Waeleze Waheshimiwa majaji wasimamizi wa uchaguzi huo katika ngazi za wilaya walikua ni akina nani Golugwa:Waheshimiwa Majaji wasimamizi walikua ni Wakurugenzi wa Halmashauri husika Lissu:Waeleze Waheshimiwa majaji wasimamizi kwenye ngazi za vituo.Golugwa:Waheshimiwa Majaji wasimamizi katika ngazi hizo za mitaa, za vijiji walikuwa ni wataendaji wa Serikali kwenye hizo ngazi za mitaa na vijijiLissu:Waeleze Waheshimiwa majajji hawa Wakurugenzi ambao umesema wamesimamia katika hizo ngazi za Halmashari hawa ni wateule wa nani?Golugwa:Waheshimiwa Majaji hawa Wakurugenzi ni wateule kwa maana kwamba wanateuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Lissu:Na Waeleze Waheshimiwa majaji huyo Waziri aliyetunga kanuni za uchaguzi huo ni mteule wa nani?Golugwa:Waheshimiwa majaji Waziri aliyetunga hizo kanuni ni mteule wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Lissu:Waeleze Waheshimiwa majaji na hiyo Wizara inayoitwa ya TAMISEMI ipo chini ya nani  Golugwa:Hiyo Wizara ya TAMISEMI ipo chini ya Ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Lissu:Kwenye ushahidi wako umesema kwamba umepeleka taarifa ya huo uchaguzi wa Serikali za mitaa wa 2024 kwa Katibu Mkuu na hao Makatibu wengine 9 wa kanda kwa mtazamo mmoja. Sasa Waeleze Waheshimiwa majaji kwa ufahamu wako huo uliouita ushenzi kwenye uchaguzi wa Serikli za mitaa kama ulikuwepo kwenye uchaguzi wa 2025.Golugwa:Mambo niliyoyaona kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa ndio hayo hayo ambayo nimeyaona kwenye uchaguzi mkuu Lissu:Waeleze Waheshimiwa majaji kwa ufahamu wako kama mambo hayo unayoyaita ya kishenzi kama uliyaona kwenye chaguzi zingine.Golugwa:Kwa kipindi ambacho nimekuwa kiongozi wa chama nimeyaona mambo hayo kwenye uchaguzi wa 2020, niliyaona kwenye uchaguzi wa mwaka 2015 na niliyaona, nikashaa, nikastaajabu mpaka nikaogopa ni kwenye matukio ya 2025.Lissu:Kwenye tatizo la kwanza la wagombea kunyimwa fomu Waeleze Waheshimiwa majaji kama uliliona kwenye uchaguzi mkuu Golugwa:Waheshimiwa majaji nimeliona na nimelishuhudia suala la wagombea katika uchaguzi mkuu, wanakwenda kuchukua fomu muhusika anakataa kutoa fomu, au anafunga mlango anaondoka anaacha ofisi Lissu:Waeleze Waheshimiwa majaji haya matatizo ambayo umeyasema hapa naomba uwaeleze Waheshimiwa majaji, haya matatizo yamekua yanawakuta wagombea wote au wagombea flani flani tu.Golugwa:Matatizo haya yamekuwa yanawakabili hasa wagombea wa Chadema na vyama ambavyo vimewahi kulalamika kadhia hii ni pamoja na ACT Wazalendo. CUF na kadhia hii haijawahi kuwapata wagombea wa vyama vingine.Lissu:Shahidi Waeleze Waheshimiwa majaji kwa ufahamu wako kuhusu mgombea yoyote wa CCM aliyewahi kuenguliwa Golugwa:Kwa ufahamu wangu sijawahi kusikia au kusoma mahali wa CCM katika nafasi yoyote kuenguliwa Lissu:Waeleze Waheshimiwa majaji kuhusu ufahamu wako taarifa za watazamaji wa nje wa chaguzi zetu Golugwa:Nafahamu taarifa za watazamaji wa nje kuhusu chaguzi zetu Lissu:Umesoma taarifa zipi Golugwa:Waheshimiwa Majaji nimesoma taarifa za Umoja wa Mataifa, nimesoma pia taarifa uliyotolewa na SADC ambayo iliongozwa na Spika mstaafu wa Malawi, nimesoma taarifa ya Umoja wa Ulaya, nimesoma taarifa kutoka taasisi ya Thabo Mbeki Foundation Lissu:Hizo ulizosoma zilikua zinahusu uchaguzi upi  Golugwa:Hizi zilihusu uchaguzi wa mwaka 2025Lissu:Sasa Shahidi Waeleze Waheshimiwa majaji hizo taarifa ulizozisoma zimesema nini wa hayo uliyoita ushenzi, wamesemaje juu ya mfumo wa Uchaguzi Tanzania Golugwa:Waheshimiwa majaji ripoti ya uangalizi wa Umoja wa Afrik ilisema, uchaguzi wa Tanzania hauna viwango na haujakidhi matakwa na viwango vya Kidemokrasia, pili Waangalizi walishuhudia wapiga kura wakipewa kura nyingi na wasimamizi wakiingiza kura kwenye masanduku ya kura nyingi na hivyo kuona uchaguzi haufai kuitwa uchaguzi.Lissu ambaye pia ni Wakili wa Mahakama Kuu na mahakama za chini yake, anakabiliwa na kesi ya uhaini akidaiwa kutenda kosa la kuitishia Serikali, kinyume na  kifungu cha 39(2) (d) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu (Penal Code – PC) Rekebu ya mwaka 2023.

Anadaiwa kuwa Aprili 3, 2025, akiwa raia wa Tanzania, kwa nia ya uchochezi alishawishi umma kuzuia kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, kwa kutamka na kuandika (kuchapisha) mtandaoni maneno ya kumshinikiza kiongozi Mkuu wa Serikali ya Tanzania.

Maneno hayo yanayodaiwa kuwa ya uhaini, Lissu alitamka kuwa : “Wanasema kitu kimoja hapa, msimamo huu unaashiria uasi, ni kweli…, kwa sababu tunasema tutazuia uchaguzi, tutahamasisha uasi, hivyo ndivyo namna ya kupata mabadiliko…, kwa hiyo tunaenda kikinukisha…, sana sana huu uchaguzi tutaenda kuuvuruga kwelikweli…, tunaenda kukinukisha vibaya sana…”

Kesi hiyo inasikilizwa na  jopo la majaji watatu, Dunstan Ndunguru akishirikiana na  majaji James Karayemaha na Ferdinand Kiwonde, Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam, imeahirishwa mpaka kesho ambapo shahidi ataendelea kutoa ushahidi wake.